Usingizi ni dawa ambayo inaweza kukutibu bila wewe kujua, kwa hiyo inafaa uitumie mara nyingi.
Ni wengi katika jamii ambao hawafahamu umuhimu wa kupata muda mzuri wa kulala katika maisha yao.
Pia,
wengi hawatambui jinsi ukosefu wa usingizi wa kutosha ulivyo na athari
kwao na kuwa kulala kwa muda mfupi kunapunguza kichochezi dume kiitwacho
testosterone.
Mwonekano wa mwanamume yeyote duniani na kupata sifa ya kuitwa mwanamume husababishwa na kichochezi hiki testosterone.
Kichochezi
hiki kiletacho tabia na maumbile ya kiume na kumpa mtu sifa ya kuitwa
mwanamume kinaweza kuathiriwa na ukosefu wa usingizi wa kutosha.
Kichochezi
hiki kinazalishwa katika sehemu za uzazi za mwanamume katika korodani
na hutiririshwa kutoka korodani na kusambaa kwenye sehemu mbalimbali za
mwili kupitia njia ya damu.
Homoni
hii ndiyo inayotoa maumbile na kazi za kimwili kwa wanaume na hufanya
maumbile ya kiume kuwa na misuli iliyo kakamavu, mifupa imara, kuota
ndevu, kupata ndevu za kifua, kuongezeka maumbile ya viungo vya uzazi,
kuwa na sauti nzito, kumfanya mtu apate hamu ya kujamiiana, kuwa na
mikono iliyojitokeza kwa nje, kutembea kibabe.
Pia, kichochezi hiki hasa kwa wanaume hutokea kuwa na upara kichwani.
Nini athari ya kupungua kichochezi hiki?
Wanaume
wengi wanapofikia umri wa miaka 30 au zaidi, wengi wao hudhani kuwa
kupungua kwa uwezo wao wa kujamiiana kunasababishwa na umri mkubwa,
kumbe sivyo.
Hilo
si sahihi, bali ni kupungua kwa kichochezi hiki cha testosterone. Moja
ya athari ya kupungua kwa kichochezi hiki ni kupungua kwa nguvu za kiume
na kutofika kileleni, kukosa mwamko wa kujamiiana, kupata ugumba kwa
wale walio katika umri wa uzazi.
Mambo
haya yakitokea humwathiri mhusika kisaikolojia na kumfanya kuwa na
sonono (depression), kuwa na tabia za ukali, msongo wa mawazo,
unyongofu, kujitenga na jamii kwa kule kuhofia kunyanyapaliwa, misuli ya
mwili kupungua uzito na uimara, huwa katika hatari ya kupata maradhi ya
moyo.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa watu wenye upungufu wa homoni hii hufa mapema kulinganisha na wale wasio na tatizo hili.
Nini kinatokea mtu akikosa usingizi?
Tafiti
za hivi karibuni zinaonyesha wanaume wengi wanaolala kwa muda mfupi
huwa na kiwango kidogo cha kichochezi hiki. Utafiti uliochapishwa mwaka
2006 katika jarida la Sleep and Sports Health uliohusisha wazee wa umri
wa zaidi ya miaka 50 unashangaza.
“Matokeo
ya utafiti wetu yanaongeza uwezekano kuwa wanaume watu wazima na wazee
ambao hupata muda mfupi sana wa kulala nyakati za usiku huwa na kiwango
kidogo sana cha homoni ya testosterone wakati wa asubuhi,” anasema
Plamen Penev kutoka Chuo Kikuu cha Chicago, Marekani.
Wakati
wa utafiti, wataalamu waliofanya uchunguzi huo walipima kiwango cha
homoni ya testosterone katika damu kila asubuhi kwa wanaume watu wazima
wenye umri kati ya miaka 64 na 74 waliojitolea kushiriki kwenye utafiti
huo.
Aidha, mtindo wao wa kulala pamoja na kupata usingizi pia vilichunguzwa kila siku kwa muda wa wiki nzima.
Matokeo
ya uchunguzi huo yalionyesha kuwa kiasi cha usingizi walicholala
kilikuwa na uhusiano wa karibu sana na kiwango cha testosterone katika
damu wakati wa asubuhi.
Wale
waliopata usingizi mzuri na kwa muda mrefu (walau saa nane) walikuwa na
kiwango kikubwa cha testosterone wakati wale waliopata usingizi wa
kubabaisha (saa nne) walikutwa na kiwango cha chini cha homoni hiyo.
Wastani wa muda wa kulala ulikuwa saa sita.
“Pamoja
na kwamba matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa urefu wa muda wa
kulala wa mtu waweza kuwa kiashiria cha mabadiliko ya homoni katika
mwili yanayohusiana na umri, matokeo ya utafiti huu yanatoa picha ya
nini kinachotokea mwilini mtu asipopata usingizi wa kutosha.
Hata
hivyo, tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha umuhimu wa uhusiano
kati ya usingizi na mabadiliko ya homoni katika mwili,” anasema Dk
Penev.
Ushauri
Ili kuimarisha kiwango cha kichochezi hiki ni vyema kuepukana na mambo yanayoweza kuingilia usingizi wako.
Kwa mfano, kuzima kompyuta, simu, taa, runinga, redio na kuacha kulala na vikuza sauti masikioni.
Tengeneza
mazingira ya chumba chako yawe na joto la wastani na uende haja ndogo
kabla ya kulala. Inafaa kuongeza muda wako wa kulala kwa saa kumi na
muhimu kula lishe bora na mazoezi ya wastani.
Kadri unavyopata usingizi ndivyo kiwango chako cha testosterone huongezeka na kuipa uimara misuli yako ya mwili.
No comments:
Post a Comment