Serikali ya Tanzania imekosoa Muungano mpya wa hiari wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda ulioundwa hivi karibuni.
Serikali ya Tanzania imeuelezea kuwa unaenda kinyume na makubaliano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hii ni ishara ya hivi karibuni kuwepo kwa mgawanyiko katika nchi wanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Wakuu wa nchi za Kenya,Uganda na Rwanda walikutana hivi Karibuni nchini Uganda ambapo walikubaliana kuanzisha miradi ya pamoja ya kimaendeleo katika nchi zao hatua ambayo haijapokelewa vema na Serikali ya Tanzania
Hii si mara
ya kwanza kuzuka tofauti katika Jumuiya hii ambayo imeundwa ikiwa ni
mara ya pili baada ya ile ya awali kuvunjika mwaka 1977 ,wakati huo
ikiwa na wanachama watatu tu yaani Tanzania,Kenya na Uganda.
Mgogoro huu
wa sasa inaelezwa kuwa chanzo chake ni mkutano wa pande tatu uliofanyika
mapema mwezi July mwaka huu nchini Uganda ambapo nchi za Kenya,Uganda
na Rwanda zilikubaliana kuungana katika kufanya miradi ya kimaendeleo ya
pamoja ndani ya nchi zao,muungano ambao unaonekana kuitenga
Tanzania,huku Burundi hivi karibuni nayo ikijiunga na Muuungano huo na
kuufanya kuwa wa nchi nne.
Tanzania
inasisitiza kuwa kulipaswa kuwepo na mazungumzo na maafikiano miongoni
mwa nchi wanachama kabla ya kuanza utekelezaji wake.
Katika
taarifa iliyotolewa na Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki imetaja
kuwa nchi hizo zimekiuka makubaliano yaliyoko kwenye mkataba wa jumuiya
hiyo.
Sekretarieti
ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye makao yake Makuu mjini Arusha
haijasema lolote tangu kuanza Muungano huo wa nchi tatu na wala
haijajibu malalamiko hayo ya Serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment