HATIMAYE mama mzazi wa Sandra Khan
maarufu Binti Kiziwi, amefunguka kuhusu madai kwamba mwanaye amenyongwa
nchini Hong Kong baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya.
Mama mzazi wa Binti Kiziwi, Rehema Selemani mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar.
Mama huyo aitwaye Rehema Selemani
mkazi wa Sinza Kijiweni jijini Dar, amesema kuwa mwanaye amefungwa miaka
mitatu na nusu na anawasiliana naye kwa njia ya simu kila baada ya
miezi miwili.
“Taarifa za mwanangu kunyongwa si za kweli bali amefungwa miaka mitatu na nusu,” alisema mama huyo.
Mama huyo amemtupia lawama rafiki wa
karibu wa Binti Kiziwi aliyemrubuni kufanya biashara hiyo ya
kusafirisha madawa ya kulevya.
Sandra Khan maarufu Binti Kiziwi.
“Sikuijua safari hiyo ya mwanangu ila nilipigiwa simu na rafiki yake wakiwa wameshafika Nairobi, Kenya,” alisema.
Kama vile haitoshi, mama huyo anamlaumu rafiki kwa kuchukua dola 5,000 za mwanaye alizokutwanazo wakati akikamatwa.
Mbali na kuwasiliana na mwanaye, mama huyo amesema Binti Kiziwi amekuwa akimtumia fedha licha ya kwamba yuko gerezani.
“Ananitumia fedha, anasema kuwa huwa wanafanya kazi wakiwa gerezani na kulipwa,” alimalizia.

No comments:
Post a Comment