
MMILIKI wa Kampuni ya Filamu ya
Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu
baada ya majirani zake kumshitaki kwenye serikali ya mtaa kufuatia tabia
ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani.
Taarifa iliyolifikia inadai kuwa,
majirani wa Wema katika eneo analoishi, Kijitonyama jijini Dar wamekuwa
wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo hicho lakini imeonekana uvumilivu
umewashinda.
“Mara kwa mara wafanyakazi wake
wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki
serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa
majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe .
Juni 26, mwaka huu Ijumaa lilifika
kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia maji yakitoka kisha kuzagaa
mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa Mtendaji wa Kata ya
Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye aligonga kwenye nyumba
ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi aitwaye Bite.
Katika mazungumzo yao, Bite
alionekana kujitetea lakini baadaye ilibainika wana makosa na akatakiwa
kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi.
Amri hiyo ilionekana kuwa ngumu kwa
Bite na wafanyakazi wenzake ambapo busara zilitumika na kiongozi huyo wa
serikali akataka walipe faini na kuwaonya waache tabia hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, Bite aliingia
ndani (inadaiwa alikwenda kumtonya Wema) ndipo alipotoka akiwa na fedha
ambazo Ijumaa halikujua ni kiasi gani, wakasainishana kisha mchezo
ukaishia hapo.
Jitihada za kumpata Wema kuzungumzia
sakata hilo ziligonga mwamba kutokana na msanii huyo kutopokea simu na
hata mwandishi alipofika nyumbani kwake aliambiwa hayupo.
No comments:
Post a Comment