Ulikuwa bado una wasiwasi na utajiri wa msanii wa Kenya Jaguar? Well,
sio mimi ni yeye ndio katoa tip ya kile alichokuwa amebebea jana jioni
kabla ya kupanda ndege kurudi nchini Kenya akitokea UK.

Katika picha aliyoiweka kulikuwa na Passport yake ili wasije kusema
alitumia picha ya mtu mwingine, then cheni moja ya gold ya hatari, saa
mbili za gharama, Samsung Galaxy note, Calvin Klein Cologne na noti za
UK pound za kutosha.
Lakini Jaguar amedhihirisha hana kigeugeu katika swala zima la
kujilinda, alikuwa na pakti moja ya condom aina ya durex, nadhani hii
ndio iliyobaki, LOL!.
Hit maker wa ‘Kigeugeu’ Jaguar alikuwa akirejea Kenya baada ya kuvuka
boda kama alivyoimba katika wimbo wake ‘Navuka boarder’ akitokea London
Uingereza ambako alitumbuiza katika show moja na TID wa Tanzania
No comments:
Post a Comment