MTANDAO wa gazeti la New Vision la Uganda umeonyesha viwango vya mishahara vya wachezaji mbalimbali wa Uganda na Zambia na kutangaza mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anapokea mshahara wa dola
10,000
kwa mwezi sawa na ( sh 15,362,000) .
Mtandao huo ulisema Okwi ni mchezaji muhimu kwa timu ya taifa ya Uganda pamoja na klabu yake ya Simba, pia anajua kufunga na vilevile ni mshambuliaji ambaye ni vigumu kumzuia.
Pia mtandao huo ulisema Okwi anajua kukimbia katika njia za kufunga na husumbua sana mabeki ndiyo maana analipwa kiwango kikubwa cha fedha na klabu yake ya Simba nchini Tanzania.
Akizungumzia taarifa hiyo Makamu Mwenyekiti wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu alisema suala la mshahara ni kitu binafsi kati ya mwajiri na mchezaji.
"Siwezi kusema Okwi anapokea kiasi gani kwa sababu hilo ni suala lake binafsi na kama ilo gazeti la Uganda limesema hivyo mimi sijui wamepata wapi taarifa hizo.
Kaburu aliongeza kusema: "Unajua unaposema Okwi anapokea kiasi fulani unaweza kumsababishia matatizo mchezaji mwenyewe pamoja na klabu kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Okwi amerejea jana jioni akitokea Uganda na kuthibisha kwamba yuko fiti kuivaa Azam hapo kesho.
Kwa mujibu wa mtandao huo mchezaji wa Zambia, Christopher Katongo anayechezea klabu ya Henan ya China analipwa kiasi cha dola 458,000 kwa mwaka na klabu yake hiyo ambazo ni sawa na (sh 703,580,000). .
Pia, Emmanuel Mayuka wa Zambia anayechezea klabu ya Southampton ya England analipwa pauni 25,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na sh .
Yupo pia kiungo wa Zambia, Isaac Chansa anayechezea klabu ya Henan ya China analipwa dola 30,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 61,479,900) .
Kiungo hatari wa Zambia, Chisamba Lungu anachezea klabu ya Sverdlovsk ya Russia, analipwa na klabu hiyo dola 25,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 38,405,000 ) .
Stophira Sunzu beki mwingine wa kati wa Zambia anayechezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, klabu hiyo inamlipa dola 20,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 38,405,000).
Rainford Kalaba kiungo wa Zambia anayechezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, ambapo klabu hiyo inamlipa dola 20,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 30,724,000) .
Wengine ni kipa Kennedy Mweene wa Zambia anayedakia klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini analipwa Rand 150, 000 kwa mwezi sawa na (Sh 28,170,400).
Dennis Onyango kipa wa Uganda anadakia klabu ya Sundowns ya Afrika Kusini na analipwa na klabu hiyo dola 15,000 kwa mwezi sawa na (sh 23,043,000) .
Mchezaji mzoefu wa Uganda, Simeon Masaba anayechezea klabu ya Dempo FC ya India analipwa na klabu hiyo dola 15,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na ( sh 23,043,000) .
Beki Henry Kalungi wa Uganda anayechezea klabu ya Richmond Kickers ya nchini Marekani, analipwa na klabu hiyo kiasi cha dola 15,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 23,043,000).
Nathan Sinkala kiungo wa Zambia anachezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, klabu hiyo inamlipa dola 15000 kwa mwezi sawa na ( sh 23,043,000) .
Kiungo Moses Oloya wa Uganda anachezea klabu ya Sai Gon ya Vietnam), klabu hiyo inamlipa dola 10,000 kwa mwezi sawa na ( sh 15,362,000) .
Beki Davies Nkausu wa Zambia anayechezea klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini analipwa na klabu hiyo dola 10,000 kwa mwezi sawa na (sh 15,362,000).
Kiungo wa Uganda, Hassan Wasswa anayechezea klabu ya Kayseri ya Uturuki, klabu hiyo inamlipa kiasi cha dola 8000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh12,289,600).
Hichaani Himoonde beki wa kati wa Zambia anayechezea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo analipwa dola 7000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 10,753,400) .
Beki Joseph Musonda wa Zambia anachezea klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini analipwa dola 5000 kwa mwezi ambazo ni sawa na (sh 7,681,000).
No comments:
Post a Comment