Ester Budili anaedaiwa kuwa ni mhasibu ingawa kwenye hati ya mashitaka haikuelezwa nafasi yake ya kazi, amepandishwa kizimbani leo na kusomewa mashitaka kumi yakiwamo ya kughushi na mmoja la wizi wa fedha hizo.
Hata hivyo baada ya kusomewa mashitaka alikana yote na kuachiwa kwa dhamana ambayo mashalti yake
ilikuwa ni wadhamini wawili wa kuaminika ajira zao, mmoja kutoa Sh milioni 45 ambapo mshitakiwa mwenyewe alitakiwa kusarenda pasi yake ya kusafiria.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Budili anadaiwa kuingiza majina ya wanafunzi ambao hayatambuliki 91 kwenye orodha ya malipo ya mikopo ya wanafunzi katika vyuo tisa.
Mashitaka hayo yalisomwa na mwendesha mashitaka Frida Mwela mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Binge Mwashabala.
Budili alidai katika siku isiyofahamika kati ya Augosti 5 na April 24 mwaka jana katika ofisi za Bodi ya mikopo iliyoko wilayani zilizoko Msasani wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akiwa mtumishi wa umma aliiba fedha mali ya mwajiri wake Sh. 90,775,800.
Shitaka la kwanza alidaiwa kughushi katika tarehe hizo hizo orodha ya majina:
- Chuo Kikuu cha Bugando: John Suzan, Peter Bahati, Mombo Yusuph, Bitaliho Gordian, Kwangaya Ibrahim, Alfred Happy, Isack Simon na Nyangige Juliana huku akijua si kweli.
- Chuo cha Uhandisi na Tecnolojia, Catherine Nkya, John Nkyaa, Andrew John, Goliama Ally, Simon Pamela, Gaash damian na Suzane John.
- Chuo cha maendeleo ya Jamii: Suzane John Meela Christopha, Zake Ezra, Goliama Ally, Simon Michael, Peter Massawe, Naruo Peter, Pamela Simon na Catherine Nkyaa.
- Chuo Kikuu cha Ualimu cha Dar es Salaam: Pamela Simon, Minisi Grace na Hamza Goliama.
- Chuo cha Ustawi wa Jamii: Pamela simon, John Suzan, Alfred Happines, Wambura Juliana, John Andrew, Andrew nkyaa, Hamza Golima na Suzane John.
- Chuo cha Tiba cha KCMC: Peter Naruo, Simon Nkyaa na Pamela Simon.
- Mzumbe: Pamela Nkyaa, John Nkyaa, Simon Andrew, Pamela Michael, Ester Goashi, Ester Damian, Daudi Ester, Adiambula Ester, Peter Bahati, Naruo Peter na Suzane John. Tumaini, chuo cha Ruaha, Hamza Goliama, Ester Lissu, Kalinga Ester, Alfred Happy, Andrew John, Pamely Michael, John Nkywimba, Pamela Simon, Suzane Nkya, John Nkuba, Catherine John, Simon Nkya, Adia Elisha, Suzane John, Naruo Peter, Ester Lucus na Adihambo Delinja. Huaha, Suzane, Paul Naruo, Michael Pamela, Bahati Peter, Dismas Ester, Lilian Victory, John Sukamule, Diambo Mbudala, Pamela John, Suzane John, Anordl Bulili, John Suzane Simon Pamela Catherine Nkyaa, Damas Ester na Simon Ngonyani.
Source:Wavuti.com
Ukiwa mhasibu ni rahisi kutupiwa dhambi zote je yeye ndiye signatories wa kutoa hizo pesa,
ReplyDeletena je aliyekuwa anasaini yeye hakufuatilia kuwa akaunti za wahusika ni sahihi au sio sahihi,
wote wawajibishwe sio kumuacha yeye tu binti wa watu