Etihad Business Studio |
Food & Beverage Manager |
Shirika la ndege la Etihad limetajwa kuwa Shirika la Ndege la Mwaka wakati wa tuzo za Business Travel 2016. Hafla hii ilifanyika jana usiku katika hoteli ya Grosvenor House iliyopo Jijini London. Tuzo hizi zinatambua makampuni na watu binafsi waliopata mafanikio katika sekta ya biashara ya usafiri na hivyo kuwafanya wastahili kuwania tuzo hizo.
Tuzo hizi zinazoandaliwa na jarida la Uingereza la Buying
Business Travel, huwa na jopo la wataalamu wanaojadiliana na kisha kupiga kura
kubaini washindi. Hii ni mara ya kwanza kwa Etihad kushinda tuzo hiyo, hii
ikija siku chache tu baada ya shirika la ndege la Etihad kupokea “Tuzo ya
Uvumbuzi katika Usafiri” kutoka tuzo za jarida la Globe Travel katika hafla
nyingine iliyofanyika wiki iliyopita London.
James Harrison, Meneja Mkuu wa shirika la Etihad Uingereza,
alisema: “Tuzo hii ni ishara ya kutambulika kwa mchango wa Etihad katika sekta
ya usafiri wa anga nchini Uingereza. Tunajisikia fahari kubwa sana kutambuliwa
katika jukwaa kubwa hivi.”
“Uingereza ni soko muhimu kwa shirika hili na mwaka huu umekuwa
na mafanikio makubwa kwetu kwani tunasherekea miaka kumi tangu tuanze kutoa
huduma zetu kati ya jiji la Manchester na Abu Dhabi. Tunategemea kuzindua
huduma ya tatu ya kila siku kutoka uwanja wa ndege Heathrow, jijini London,
kupitia ndege aina ya A380 ambayo pia ina huduma ya vyumba ya “Makazi”. Zaidi
tunalenga kutoa huduma iliyorahisishwa na inayowaunganisha wageni wetu.”
Shirika la Etihad liliibuka kidedea kutokana na huduma zao za
hali ya juu, zikiwemo bidhaa (na vyumba) zilizoingia hivi karibuni sokoni na
kuleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa anga. Hii ikiwa pamoja na kutumia
ndege aina ya Airbus A380 na Boeing 787 Dreamliners, bila kusahau vyumba
ambavyo vilishakuwa vikitumika na Airbus A330/A340 na Boeing 777.
Mapinduzi haya yametokana na programu ya utafiti na maendeleo
iliyoendeshwa katika Kituo cha Uvumbuzi kilichopo Abu Dhabi na kuongozwa na
timu ya ubunifu ya Etihad. Shirika la Etihad linapenda kutoa huduma yenye
viwango sawa na hoteli kubwa na sehemu nyingine za kitalii kubwa duniani. Etihad
wameajiri wafanyakazi wenye ufundi na uzoefu mkubwa haswa katika safari ndefu
kwa mfano wahudumu wakuu walipo katika “Makazi” ya ndege ya A380 kwenda London,
Wapishi Wa daraja la Kwanza, meneja wa vyakula na Vinywaji katika “daraja la
biashara” na wahudumu wa kutunza watoto wakati wa safari. Wahudumu hawa
wamehitimu chuo cha kulea na kutunza watoto Norland huko Uingereza.
Pia shirika la ndege la Etihad lina sehemu ya mapumziko
katika viwanja vya ndege wa London Heathrow, Manchester, Frankfurt, Dublin,
Paris, Sydney, Washington, D.C. na New York wakati uwanja wa ndege wa Abu Dhabi
una sehemu za mapumziko na mapokezi.
No comments:
Post a Comment