Ndege ya uzinduzi ya Shirika la Ndege la Etihad ikipokelewa na magari ya zimamoto ambayo yalimwaga maji kuashiria uzinduzi rasmi wa Safari za ndege kati ya Rabat na Abudhabi. |
ETIHAD YAZINDUA HUDUMA ZA SAFARI ZA NDEGE KUFIKA MJI
MKUU WA MOROCCO, RABAT
Safari kati ya
Abu Dhabi na Morocco kufikia tisa kwa wiki
Shirika
la ndege la Etihad lazindua rasmi huduma zake za ndege baina ya Abu Dhabi na
Rabat, Morocco, ikiwa ni kituo chao cha pili nchini humo.
Ndege
ya uzinduzi iliwasili mchana wa leo uwanja wa ndege Sale-Rabat na kupokelewa na
mzinga wa maji kama ilivyo desturi ikifuatiwa na wageni rasmi kuwasili,
wakiwemo; Lahcen Haddad (Waziri wa Utalii Morocco), na Balozi wa UAE kwa
Morocco, Mh. Al Asri Saeed Al Dhaeri.
Huduma
hii itakayopatikana mara mbili kwa wiki kupitia ndege aina ya Airbus A340-500
itakuwa yakipekee baina ya Rabat na Abu Dhabi. Tayari kukiwa na safari baina ya
Abu Dhabi na Casablanca, shirika litafikisha jumla ya safari tisa kwa wiki
kwenda nchini Morocco
Ndege
ya uzinduzi (EY615) kwenda Rabat ilibeba msafara ulioongozwa na Khaled Al
Mehairbi, Makamu Rais Mambo ya Serikali na Siasa za Anga. Uwakilishi huu
ulijumuisha Kapteni Salah Awadh Alfarajalla, Makamu Rais Usalama na Maaendeleo
ya Waendesha Ndege Kitaifa; Hareb Mubarak Al Muhairy, Makamu Rais Mambo ya
Mashirika na Kimataifa; Ali Al Shamsi, Makamu Rias Operesheni za Kitovu cha Abu
Dhabi; Joost Den Hartog, Kaimu Makamu Rais wa Mauzo Duniani; na Amer Khan,
Makamu Rais Mashariki ya Kati na Africa Kaskazini.
James
Hogan, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Etihad, alisema shirika limefurahishwa na
uzinduzi wa huduma ya Rabat kama kituo cha pili katika safari za Morocco.
“Safari
hizi mpya zitakazounganisha miji hii zinadhihirisha dhamira ya Etihad kuendelea
kujenga mahusiano endelevu na kanda ya ksakazini mwa Afrika na kuimarisha
uhusiano kati ya Morocco na Umoja wa Falme za Kiarabu,” alisema.
“Rabat
ni mji wa kihistoria unaovutia wanaosafiri kwa ajili ya burudani na biashara.
Kwa kupitia huduma yetu mpya, tunalenga kutumia mtandao wetu uliopo duniani
kote kukuza wingi wa wasafiri wataotumia njia hii kuingia Morocco. Vivyo hivyo
tunarahisisha safari katika Rabat hadi Abu Dhabi pamoja na miji mingine tunayofika,
huku tukiwapa wageni wetu fursa ya kufurahia huduma zetu za viwango vya juu
zinazotambulika dunia nzima.”
Pamoja
na Casablanca, huduma hii ya Rabat itafikisha jumla wasafiri 4,200 kila wiki
kwenda Morocco.
Kama
UAE, serikali ya Morocco imewekeza sana katika kuiendeleza sekta ya utalii.
Mwaka 2010, serikali ilizindua Vision 2020 ikiwa na mpango wa kuifanya Morocco
kuwa kati ya sehemu kuu 20 za utalii duniani na hii itachangia kuongeza idadi
ya watalii hadi mara mbili ya idadi ya awali hadi kufikia takribani milioni 20
mpaka kufika mwaka 2020.
Balozi wa UAE kwa Morocco, Mh. Al Asri
Saeed Al Dhaheri, alisema: “Sina mashaka kwamba safari hizi kati ya miji hii mikuu
ya kiarabu zitaimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi katika masuala ya usafiri
wa anga. Hii ni hatua nyingine ya maendeleo katika uhusiano kati ya UAE na
Morocco. Safari za moja kwa moja zitachangia sana kuleta maendeleo katika
biashara, uwekezaji na utalii. UAE na Morocco zimeunganishwa na historia ndefu
ya ushirikiano na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizi mbili na
utaendelea hivyo katika miaka ijayo.”
“Nimeridhika sana kwa kampuni za UAE
zinavyozidi kutazama kwa umakini nafasi zilizopo kushirikiana, kuwekeza na
kufanya biashara mjini Rabat. Ni dhahiri kwamba nyakati zijazo jamii za
kibiashara zitapata faida kubwa katika nchi hii na tungependa kushuhudia
ushirikiano ukikua na bila shaka shirika la Etihad ni mfano mzuri wa hili.”
Huduma hii itakuwepo Jumatano na Ijumaa kwa kutumia
ndege aina ya Airbus A340-500 yenye siti 240, 12 za
daraja la kwanza, 28 za daraja la bisahara na 200 za daraja la uchimi.
Huduma ya Abu
Dhabi-Casablanca imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanzishwa Juni mnamo mwaka 2006.
Huduma ya Abu Dhabi-Rabat inawapa abiria chaguo zaidi na njia mbili zinazounganisha
Morocco na UAE na imefungua njia kufika sehemu nyingine katika mtandao wa
Etihad’ GCC, Bara la Hindi na Asia Kusini Mashariki pamoja na Australia
Shirika la Etihad
pia limesambaa kufika Afrika Kaskazini kwa makubaliano ya ‘codeshare’ na Royal
Air Maroc, ikiwapa abiria ndege za safari za moja kwa moja kutoka Casablanca
mpaka sehemu zingine Morocco kama Agadir, Marrakech and Tangier.
Shirika
la ndege la Etihad pia imeongeza huduma zake Afrika kufika Johannesburg,
Khartoum, Cairo, Lagos, Nairobi, Entebbe, Dar es Salaam and Mahé in the
Seychelles.
Ndege na.
|
Kuondoka
|
Kuwasili
|
Muda wa kuondoka
|
Muda wa kuwasili
|
Aina ya ndege
|
Siku
|
EY 615
|
Abu Dhabi
|
Rabat
|
10.00
|
15.15
|
A340-500
|
Jumatano/Ijumaa
|
EY 616
|
Rabat
|
Abu Dhabi
|
20.00
|
07.25 kesho yake
|
A340-500
|
Jumatano/Ijumaa
|
Angalizo: muda wa kuondoka na
kuwasili ni kwa muda wa Abu Dhabi
Kuhusu
Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege
la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014,
ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko
Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri
na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia,
Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing
takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66,
Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza
katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin
Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya
biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin,
Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia
hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta
kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora
zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja
wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.comsoma zaidi hapa www.darwaya.com
No comments:
Post a Comment