27 December 2015

SAMATTA AIPA SIMBA SH 1.2 BILIONI

Na Karim Boimanda
KUNA msemo mtaani unasema 'Unaweza kulala masikini akaamka tajiri'. Huo unaitokea klabu ya Simba ambayo muda si mrefu italamba kitita cha Sh 1.2 bilioni.



Matajiri wa DR Congo, TP Mazembe wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa straika wao Mbwana Samatta kwenda KRC Genk inayoshika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Ubelgiji. 

Kama Genk watakubaliana na dau la Euro 2.5 milioni (zaidi ya Sh.6 bilioni) analotaka tajiri Moise Katumbi basi ule mkataba ambao Mazembe walimpa Samatta una makubaliano ya kuilipa Simba asilimia 20 mara mchezaji huyo atakapouzwa akitokea Mazembe.

Akizungumza na BOIPLUS, Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' ambaye ndiye alisimamia mauzo ya Samatta kwenda Mazembe alisema Mazembe wanapaswa kulipa asilimia 20 ya pesa watakayopata kwenye mauzo ya Samatta.

"Mkataba unasema ni asilimia 20, sisi tunachosubiri ni huu mpango kukamilika halafu tukabidhiwe chetu,'' alisema Kaburu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname