Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano linaanza leo Dodoma kwa kusomwa Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge, uchaguzi na Kiapo cha Spika, Kiapo kwa wabunge woteMuda huu tayari wabunge wameanza kuwasili kwenye viwanja vya Bunge na wengi wamo kantini hapa wakipata staftahi kabla ya kuingia rasmi ukumbini.

Update.
Wabunge wengi wanaingia bungeni now harakaharaka maana mida wowote Kikao kitaanza. Changamoto iliyopo ni kuwa.baadhi ya wabunge hasa wapya wamevaa mavazi ambayo sio ya kibunge jambo ambalo ni kinyume na kanuni. Labda ugeni utawaokoa wasitolewe nje

Updates
Katibu wa Bunge Dr Kashililah ndio anaanza kwa kusoma tangazo la Rais kuitisha bunge la 11. Mkutano wa uchaguzi unaanza na Andrew chenge anateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika. Chenge kaingia na uchaguzi unaanza kwa wagombea kuitwa kujieleza

Updates
Wagombea wote wameruhusiwa kuingia ndani na wameingia ukumbini isipokuwa Hashim Runngwe ingawa hajajitoa hivyo anaruhusiwa kupigiwa kura bado

Updates
Wagombea wametoka nje na wanaitwa mmojammoja kujieleza kwa dakika tatu na maswali matatu kama yapo