Umesema staili watakayoitumia ni tofauti na ile waliyoitumia wakati Rais
wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alipozindua Bunge la 10 mwaka 2010 ya
kutoka nje ya ukumbi kuonyesha kutotambua serikali yake.
Akizungumza na mtandao huu katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana,
aliyekuwa Mnadhimu wa Bunge la 10 Kambi la Upinzani Bungeni, Tundu
Lissu, alisema safari hii hawatatoka nje ya ukumbi wa Bunge hata kama
hawamkubali Rais Magufuli, kwa kuwa ni wajibu wao kushiriki vikao vya
chombo hicho cha kuwakilisha wananchi.
“Sisi ni wabunge, tumo humu kwa ridhaa ya wananchi, tuna haki ya kuingia
bungeni, hivyo siku hiyo tutaingia lakini kitakachotokea tutajua siku
hiyo, bali haitakuwa kama walivyotuzoea tunatoka nje,” alisema na
kuongeza:
“Subira yavuta heri, bado siku tatu tu, Watanzania watajua msimamo wetu tukiwa ndani ya Bunge,” alisema.
No comments:
Post a Comment