Njemba huyo akionekana kurandaranda kwenye Maduka ya Mlimani City.
Boniphace Ngumije na Brighton Masalu
Taharuki! Katika
hali ya kushtua, njemba mmoja mtata mwenye asili ya Kiarabu amezua
tafrani kwenye Maduka ya Mlimani City yaliyopo Barabara ya Sam Nujoma,
jijini Dar baada ya kudakwa akitalii na kupiga picha za mnato kwenye
maeneo maalum bila kujulikana lengo lake.
...Akikatiza kwenye vikordo
Kwa mujibu wa shuhuda wetu,
sekeseke hilo lilijiri kwenye maduka hayo mapema wiki hii, majira ya
mchana ambapo jamaa huyo aliyekuwa na ‘mandevu mengi na marefu’ alitinga
mahali hapo huku akiwa amevalia mavazi meusi tii.
Akiwa kwenye korido za
maduka hayo, mtu huyo alianza shughuli ya upigaji picha aliyokuwa
anaifanya kwa tahadhari kubwa kwa kutumia kifaa maalum chenye umbile la
kamera za dijitali.
“Jamaa alikuwa akizunguka
sehemu maalum alizopanga kuzifanyia kazi bila kuogopa sheria ambazo
haziruhusu mtu kupiga picha maeneo hayo.
Kwa mbali akitokomea chooni.
“Baadaye alitiliwa shaka kutokana na watu kuingiwa hofu juu yake kwani baadhi walikuwa wanamkimbia ndipo akadakwa na walinzi.
“Walinzi wa Mlimani City
walipomkamata walimhoji kwa nini anapiga picha, akasema alikuwa
analinganisha uzuri wa maduka hayo na huko kwao alikotoka,”alisema
shuhuda.
Baada ya kuudaka ubuyu huo,
timu ya waandishi wetu iliingia kazini na kuelekea moja kwa moja
Mlimani City kuzungumza na Meneja Mkuu wa maduka hayo, Pastory Mrosso
ambaye alisema:
“Ni kweli tukio hilo
limetokea lakini lilikuwa ndani ya uwezo wetu wa vyombo vya usalama
tulivyonavyo maana jamaa hakuchukua muda mrefu kufanya hivyo, alikamatwa
na kuhojiwa. Baadaye aliamuriwa kuzifuta picha hizo kisha aliachiwa
huru.”
No comments:
Post a Comment