16 November 2015

NIKO INSURANCE LIMITED YABADILI JINA NA KUWA SANLAM GENERAL INSURENCE

 Afisa Mtendaji Mkuu wa iliyokuwa NIKO Insurance Bw. Manasseh Kawoloka akizungumza mbele ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya kubadilisha jina la kampuni hiyo ambapo sasa inaitwa Sanlam General Insurance.hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Afisa Mwandamizi wa Ukuaji wa Mashirika wa Sanlam Emerging Markets (SEM) Ndugu Thabied Majaj  akitoa Hotuba yake kwenye halfa ya Kampuni ya NIKO Insurance Limited ilipobadili jina na kuwa Sanlam General Insurance

Kampuni ya Bima ya Niko imebadili jina na kuwa Sanlam General Insurance. Mabadiliko hayo yanalenga kupanua wigo na kuimarisha uwepo wake nchini Tanzania na Afrika Mashariki  kwa ujumla. Sanlam General Insurance itaendelea kutoa huduma mbalimbali za bima kwa wateja binafsi na mashirika nchini Tanzania. Huduma za Sanlam General Insurance ni pamoja na za biashara na binafsi kama vile Magari, Moto na nyinginezo.

   Sanlam Group  yenye makao makuu yake nchini Afrika Kusini inamiliki asilimia 46 ya hisa za NIKO (Sasa Sanlam General Insurance), kupitia kampuni yake tanzu ya Masoko Yanayokua yaani Sanlam Emerging Markerts (SEM).
Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam General Insurance (zamani NIKO Insurance) Bw. Manasseh Kawoloka, Afisa Mwandamizi wa Ukuaji wa Mashirika wa Sanlam Emerging Markets (SEM) Bw. Thabied Majal, Kamishna Msaidizi wa TIRA Bw. J.J Makame na Wajumbe wa Bodi ya Sanlam General Insurance Tanzania Ltd, Mh. Joseph Mungai, Bw. Naftal Nsemwa na Bw. Nelius Bezudeinhoud katika  hafla ya uzinduzi wa jina jipya la kampuni ya bima ya NIKO ambayo sasa inaitwa Sanlam General Insurance Tanzania Ltd iliyofanyika tarehe 11 Novemba 2015 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.


Afisa Mwandamizi wa Ukuaji wa Mashirika wa Sanlam Emerging Markets (SEM) Bw. Thabied Majal alisema kuwa Sanlam Group ni Kampuni yenye sifa kubwa Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla, hivyo mabadiliko ya NIKO Insurance kuwa Sanlam General Insurance  utaleta ufanisi wa hali ya juu pamoja utendaji wa kibiashara kwa kampuni hiyo. Akieleza zaidi alisema watanzania  sasa watapata nafasi zaidi ya kupata aina mbalimbali za bidhaa za bima zenye ubunifu kufidia majanga binafsi na ya kibiashara.


Kampuni ya iliyobadili jina (NIKO Insurance) Sanlam General Insurance  inatoa huduma mbalimbali za bima katika wigo mpana kwa wateja  binafsi pamoja na Mashirika  nchini Tanzania. Huduma zitolewazo na kampuni ya bima ya Sanlam General Insurance  zinalenga biashara na watu binafsi kama Magari, Moto, Uhandisi pamoja na Bima Maalum. Kabla ya kubadili jina kampuni ya NIKO Insurance imekuwa ikitoa huduma nchini tangu Mwaka 2005.
Mjumbe wa Bodi ya Sanlam General Insurance (zamani NIKO Insurance) Ndugu Joseph Mungai  akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
Mabadiliko ya NIKO Insurance Limited kuwa Sanlam General Insurance  yanafuatia mabadiliko ya kampuni ya African Life Assurance ya Tanzania na kuwa Sanlam Life Insurance Agosti 2015. Sanlam General Insurance  inatoa utaalamu na uzoefu wa hali ya juu kwa wateja wake pamoja na wadua wengine wanaofanya kazi na kampuni hiyo.


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname