15 November 2015

A TO Z YA KIFO CHA KIGOGO WA CHADEMA MKOA NA MBINU ILIYOTUMIKA KUMUA KINYAMA GEITA NDIVYO ILIVYOKUWA HIVI.

Enzi za uhai wake, Alphonce Mawazo.
Geita. Mji wa Geita umezizima kwa simazi, vilio na majonzi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita, Alphonce Mawazo kuuawa kinyama kwa kushambuliwa na silaha za jadi ikiwamo kukata kichwa kwa shoka.
Wananchi na wafuasi wa Chadema walifurika katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Geita, wakionekana wenye nyuso za huzuni.
Mawazo (pichani) alifariki dunia baada ya kudaiwa kutekwa na kundi la watu hao wanaosadikika kuwa ni wafuasi wa chama kimoja cha siasa wakiwa na marungu, mapanga na shoka.  

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname