10 October 2015

ZARI THE BOSS LADY DIAMOND PLATINUMS BIASHARA IMIKWISHA,MAZITO YAFICHUKA

 Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
BIASHARA imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond apate mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah’ miezi miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao, kimesema makubaliano ya awali baina ya wazazi hao, yalikuwa ni kwa mwanamke huyo raia wa Uganda, kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa akisaka ubaba kwa udi na uvumba.  


No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname