Katibu
Mkuu wa Baraza la Mahedhebu kwaajili ya Amani,Mchungaji,Canon Thomas
Godda akizungumza katika kongamano la Amani lililoandaliwa na shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,Sayansi na Utamaduni
(UNESCO)kwa kushirikiana na madhehebu ya Dini na Viongozi wa Mila ili
kuhamasisha amani katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Na Mwandishi wetu, Simanjro
Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) limekutanisha wadau mbalimbali katika kongamano la kujadili na
kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 4,2015
Kongamano
hilo lilifanyika katika Kituo cha Redio Orkonerei (ORS)Terrat wilaya ya
Simanjiro mkoa wa Manyara na kuwaleta pamoja viongozi wa dini,mila na
wawakili wa muungano wa Redio za Jamii nchini(Comneta)ambao kwa pamoja
walisisitiza umuhimu wa amani.
Ofisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la
Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph alisema
mchango wa unaotolewa na Redio za kijamii nchini ni mkubwa kwani
unawawezesha wananchi kuzitumia kujiletea maendeleo katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ya kuhamasisha amani na utulivu katika kipindi hiki
na baada ya uchaguzi mkuu.
Ameongeza
kuwa Muungano wenye nguvu wa Redio za Jamii ndio ukombozi wa wananchi
kwani wanahitaji kuelimishwa maswala mbalimbali ya afya, kilimo na
programu zinazoandaliwa na serikali kwajili ya wananchi.
Mmoja
wa viongozi wa mila ,Laigwanani Lesira Samburi alisema viongozi wa mila
licha ya mchango wao kwenye jamii bado hawajashirikishwa ipasavyo
pamoja kuwa huwa hawajishughulishi na siasa moja kwa moja.
"Naomba
serikali itambue mchango wetu katika kutatua migogoro na kuhamasisha
amani kwenye jamii zetu,tunaweza kufanya mambo makubwa kama serikali
ikitushirikisha ipasavyo sio katika kipindi hiki cha uchaguzi tu bali
hata baada ya uchaguzi,"alisema Samburi
No comments:
Post a Comment