Prof. Kitila Mkumbo Awarushia Dongo Mwalimu Nyerere Foundation, Adai Waache Kuchanganya Wananchi...Soma Hapa
"Nimefuatilia kwa kiasi mazungumzo ya ndugu Butiku, Mama Mongela na
Ndugu Polepole. Nayaita mazungumzo na sio mdahalo kwa sababu hapakuwa na
hoja kinzani.Hata hivyo nina angalizo. Kwa takribani miaka kumi tangu
JK aingie madarakani Mwalimu Nyerere Foundation walikuwa vinara wa
kuinanga CCM na kutuonyesha jinsi chama hiki kilivyobadilika na kuwa cha
ovyo. Mimi naamini mlimaanisha na wala hamkuwa na chuki binafsi na JK.
Sasa itakuwa vizuri mkatueleza watanzania wenzenu ni lini hasa chama
hiki kiliacha yale mabaya mliyotueleza katika miaka kumi
iliyopita.Anyway mna haki ya kubadilika kwa sababu tumeambiwa hiki ni
kipindi cha mabadiliko. Lakini naomba sana baada ya uchaguzi msitumie
MNF kutuhubiria tena ubaya wa CCM. Tafadhalini sana, msichanganye tena
wananchi kwa kutumia taasisi takatifu ya Mwalimu Nyerere".
Ameandika hivyo Prof. Kitila Mkumbo ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam
Nini maoni yako hapo?
No comments:
Post a Comment