Mayasa mariwata
Mjengo
wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.Kwa mujibu wa chanzo
makini, Lulu na mama yake walifikia uamuzi wa kuupiga bei mjengo huo
uliopo maeneo ya Kimara Saranga jijini Dar baada ya kuona mazingira ya
eneo hilo si mazuri hususan kipindi cha mvua kutofikika kwa urahisi.
“Wamedhamiria
kuipiga bei nyumba hiyo lakini wanashindwana na wateja kutokana na pesa
hiyo ndefu anayoitaka wakati kiuhalisia nyumba haina hadhi.
“Isitoshe
ile nyumba ndani inapasukapasuka sakafu huenda kwa sababu ilianza
kujengwa siku nyingi, hivyo wateja wengi wanakwamia shilingi milioni 35
wengine milioni 40, pesa ambayo Lulu na mama’ke hawapo tayari kuipokea,”
alisema mpashaji huyo.
Elizabeth
Michael ‘Lulu’.Kutokana na ishu hiyo paparazi wetu alimtafuta Lulu
ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini mama Lulu alipotafutwa
kuzungumzia ishu hiyo alisema:
“Hii
nyumba ni yetu hata kama tukiiuza kwani kuna tatizo gani sioni kama
kuna cha ajabu hapo mpaka mkae mnatufuatilia kiasi hicho, nimeshasema
hayo ni mambo yetu binafsi hayawahusu sababu hamkutusaidia kujenga,
nimetoka msibani bado nina majonzi sitaki kuongelea tena hayo mamboº.”
No comments:
Post a Comment