Mwonekano wa gari aina ya Toyota Duet lililoungua.
GARI aina ya Toyota Duet
limeungua mchana wa leo maeneo ya Sinza Kijiweni jijini Dar ambapo
mashuhuda wa tukio hilo wemesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni kutokana
na hitilafu ya moto ulioshika tanki la mafuta wakati gari hilo likiwa
gereji.
Kamera yetu ilishuhudia gari hilo likiwa tayari
limekwishakuungua pembezoni mwa barabara eneo la Sinza Kijiweni ambapo
ilielezwa kuwa mara baada ya kushika moto taki la maufuta likiwa kwa
mafundi gereji lilikokuwa likichomelewa sehemu iliyokuwa imeharibika
waliamua kulisukuma hadi barabarani kwa ajili ya kuepusha magari mengine
kutokushika moto.
Baadhi ya wananchi wakilishudia gari hilo lililoungua moto.
Mmoja wa askari akionekana eneo la tukio.
Wananchi wakiendelea kushudia tukio hilo la kuungua kwa moto gari hilo.
Askari Trafiki akionekana kupima ajali hiyo.
No comments:
Post a Comment