MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khery Sameer, maarufu Mr. Blue,
ameweka wazi namna alivyombadilisha kimaisha mke wake, Warda baada ya
kumtoa kwenye klabu za usiku.
Mr. Blue, anayetamba na wimbo wa ‘Baki na Mimi’, alisema wimbo huo
unaeleza maisha halisi ya yeye na mke wake huyo tangu walipokutana hadi
walivyoishi na kufikia maamuzi ya kuoana na kuanzisha familia ambayo kwa
sasa wana watoto wawili.
“Wimbo huu unagusa maisha ya mimi na mke wangu Warda kwa asilimia kubwa,
wengi hawajui kuwa mke wangu nilikutana naye klabu mazingira ambayo
wengi wanadhani si mazuri kwa mwanamke, lakini kwangu ni tofauti kwa
kuwa mke wangu ana sifa zote za kuwa mke,” alisema Mr. Blue, ambaye yupo
katika maandalizi ya kuweka wimbo huo katika picha za video

No comments:
Post a Comment