Lowassa ameweza kuwateka mpaka wasomi, watu ambao unategemea wanaweza kuchambua na kutathmini kinachotoka kwenye mdomo wake. Lakini kwa wale wasiomjua vizuri Lowassa, picha kwao kidogo ni tofauti.
Mawazo yake hayo yalikuwa hivo mpaka alipoamua kwenda kwenye campaign za Lowassa pale Kigamboni hiyo jana. Ndugu yangu huyu alishangazwa sana na Lowassa 'mwenyewe'. Alitegemea kukutana na kiongozi anayejua kuongea na watu wake na mwenye kumwaga sera za maana.
Ndugu yangu anasema 'nimeona watu wanamshangilia kama 'wehu'. Hata kwa maneno ambayo hayasikiki vizuri na wakati mwingine kwa maneno yasiyokuwa na msingi.
Anasema 'kama kweli Lowassa ni mwanasiasa...mbona hata kuongea hajui?' Mimi sikumjibu...ila katika tafakari zangu nikaona kweli picha ya Lowassa iliyojengwa haendani na yeye mwenyewe. Amewekwa juu sana kuliko anapostahili. Huwa najiuliza hivi huyu mtu anasujudiwa kwa kipi hasa au amepata 'zali la mentali'?
By Mugisher

No comments:
Post a Comment