Jimbo la Makambako
ALIYEKUWA mbunge wa Jimbo la Njombe Kaskazini, Deo Sanga Maarufu kwa jina la Jah People yupo katika nafasi ya kurudi bungeni baada ya kuibuka mshindi wa kura za maoni za jimbo jipya la Makambako.
Alipokuwa akigombea mwaka 2010, Sanga atakumbukwa kwa namna alivyokuwa akiinadi elimu yake ya msingi kwa wapiga kura wake.
"Mimi ni msomi wa elimu ya juu ya msingi ndio maana ni mfanyabishara mkubwa niliyeajiri wasomi wanaosikiliza maelekezo yangu," hiyo ni moja ya nukuu zake.
No comments:
Post a Comment