02 August 2015

JOKATE AFANYA VURUGU KUBWA USIKU NYUMBANI KWAO OYSTERBAY

Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ anadaiwa kufanya vurugu nyumbani kwao usiku baada ya kutwaa Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike 2015 katika tuzo zilizotolewa na waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu (ZIFF) hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Habari kutoka kwa chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu
wa staa huyo wa sinema na Bongo Fleva zilieleza kuwa, awali Jokate ambaye hakwenda Zanzibar, hakujua chochote kuhusiana na tuzo hizo hivyo alipopewa taarifa na mtu ambaye alikuwepo kwenye tamasha hilo, alishindwa kujizua na kuanza kutimua mbio ovyo huku viatu akiwa ameviacha katika mgahawa aliokuwa amekaa jirani na nyumbani kwao, Oysterbay jijini Dar.
“Unajua Jojo (Jokate) alikuwa hajui kuhusiana na tuzo hiyo, alikuwa amekaa kwenye mgahawa mishale ya saa 3:00 usiku, jirani na nyumbani kwao.
“Alipoambiwa ameshindwa ndiyo akakimbilia nyumbani na kuanza kubamiza mageti na kutupatupa vitu, jambo lililosababisha taharuki nyumbani hapo na kusababisha wazazi wake kuhofu wakijua labla mtoto wao amepata kichaa,” kilisema chanzo hicho.
Kilisema kwamba, baada ya kuulizwa kulikoni kupagawa kiasi hicho ndipo akafunguka kuwa siyo kwamba alichanganyikiwa bali ilikuwa ni furaha ya kutwaa tuzo hiyo.
Gazeti hili lilipomtafuta Jokate alikiri kutokea kwa hali hiyo na kusema kuwa alipata mshtuko mkubwa na furaha kwa kuwa hakutegemea jambo kama hilo.
“Ukifanya kitu watu wakakukubali ni furaha kubwa na unapata moyo wa kufanya zaidi na zaidi,” alisema Jokate.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname