Mwili wa marehemu ukiwa umepakiwa ndani ya gari ya polisi
Watu wasiojulikana wamemuua mlinzi wa mahakama ya Kingulwira mjini Morogoro kwa kumkata panga kichwani na kunyofoa baadhi ya viungo na kisha kutupa mwili wake katika mashamba ya pangawe mjini Morogoro.
EATV imefika katika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa umeharibika vibaya huku baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa ambapo kwa mujibu wa mashuhuda na ndugu wa marehemu wamesema mtu huyo alipotea nyumbani takribani siku kumi na mbili zilizo pita hadi alipo okotwa na wachunga ng`ombe akiwa ameuawa na mwili wake ukiwa umeharibika.
No comments:
Post a Comment