Kama wewe ni msichana na umeshavuka miaka 30 bado hujaolewa na wala huna
mtu wa kueleweka ambaye amejitambulisha kwenu tambua kwamba una hali
mbaya.
Wasichana wengi siku hizi wamekua na tabia ya kupenda vitu vya anasa
hali inayopelekea sisi wanaume kuwaogopa kama ukoma.Mfano kutaka
kufanyiwa shopping za bei mbaya,kumiliki simu za gharama zinazoanzia
milioni moja na kuendelea,kupenda kuwa na mwanaume mwenye mshahara
unaoanzia milioni tatu kwa mwezi na kuendelea n.k
Hali hii inasababisha hata sisi wenye kipata cha laki saba kushuka chini
tuwaogope kwa kuamimini kwamba hatuna uwezo wa kukidhi mahitaji yenu
hatimaye mnajikuta mnazeekea nyumbani kutaamakitaamaki miaka 45 hii hapa
ambapo ndo kipindi cha menopause kwa mwanamke yeyote.
Msipende mteremko sababu hata huyo mwenye magari,majumba na kipato
kikubwa hujui ametumia njia gani mpaka kupata hivyo vitu.Starehe hazina
mwisho hivyo unapobweteka na starehe fahamu kwamba fainali uzeeni muda
ndio refa

No comments:
Post a Comment