Katika kipindi cha Asubuhi cha cha jana ITV alialikwa Askofu wa kanisa Katoliki ambaye alinishangaza kwa jambo jipya.
Alisema wala tusishangae yanayo fanywa na serikali ya CCM ni matokeo ya
Mwalimu Nyerere kwenda kwa mashehe fulani wa Bagamoyo ambao walifanya
tambiko ili Nchi ipate uhuru chini ya mwalimu Nyerere kwa kibali cha
mizimu.
Kusema ukweli hata mimi niliwahi kumsikia Mwalimu akisema hao wazee
walimwambia aruke shimo moja lililo fanyizwa dawa kisha akaambiwa
mkoloni hakuwezi.
Sasa kwa mjibu wa mtumishi huyo wa Mungu anasema hata Uhuru ulipo
patikana nchi ili kuwa chini ya laana kubwa kiasi kila jitihada zilikuwa
zikienda mrama daima.
Yeye ansema ameoteshwa juzi tu kuhusu mkasa huo na kuambiwa Watanzania
wasipotubu tuta kuwa tuna shuhudia viongozi wetu wakifanya vituko.
Aliongeza kuwa tabia ya mtu aliye laaniwa inajulikana anakuwa haelewi anafanya nini.Mkimlaumu atakuwa ana washangaa ninyi.
Anasema madudu yote ya CCM mathalani kutoa nguzo za umeme toka mafinga
kupelekaKenya na kisha kurudisha Nchini kwa kununua kwa fedha za kigeni
ni jambo linalo weza kufanywa na waliolaaniwa tu.
Chanzo: ITV

No comments:
Post a Comment