20 May 2015

Wageni waalikwa sherehe ya Liverpol wamzomea Sterling



Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa tuzo za msimu za klabu ya Liverpool iliyofanyika usiku wa kuamkia hii leo walisikika wakimzomea mshambuliaji wa klabu hiyo Raheem Sterling baada ya kutajwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo.
Sterling ameingia katika chuki na baadhi ya mashabiki wa Liverpool, kufutia msimamo wake wa kutaka kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na kwenda mahala pengine ambapo anahisi patampa changamoto mpya wa kusaka mataji.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20, alionyesha kutojali kelele za kuzomewa na baadhi ya mnashabiki waliokau wamefurika katika ukumbi wa Echo Arena ambapo ilifanyika hafla ya utoaji wa tuzo za msimu wa 2014-15 kwa wachezaji wa Liverpool.
Mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya mchezaji boira mwenye umri mdogo, Sterling alizungumza maneno machache ya kuwashukuru mashabiki pamoja na wachezaji wenzake kwa ushirikiano mkubwa waliomuonyesha na kasisitiza juhudi za maarifa aliyoyaonyesha uwanjani yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na benchi zima la ufundi chini ya meneja Brendan Rodghers.
Mapema hapo jana Sterling alithibitisha rasmi kuwa tayari kuondoka Liverpool mwioshoni mwa msimu huu, huku klabu za Manchester City, Arsenal, Bayern Munich pamoja na Real Madrid zikitajwa kumuwania.
Wakati huo huo kiungo mshambuliaji kutoka chini Brazil Phillipe Coutinho amatangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka, mchezaji bora wa kikosi cha kwanza, mfungaji bora wa goli la mwaka pamoja na mchezaji aliyeonyesha kiwango cha juu kwa mwaka.
Fara Williams ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kikosi cha Liverpool upande wa wanawake, huku Chris Anders akitwaa tuzo ya jamii iitwayo Bill Shankley Community Award:
Tuzio ya mchezaji bora bora wa kituo cha kuendeleza na kukuza vipaji kwa vijana imechukuliwa na kinda Joao Carlos.
Tuzo ya kikundi bora cha ushangiliaji imekwenda kwa OLSC London

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname