20 May 2015

Lucy Avunja Ukimya Kuhusu MUME WA UWOYA BWANA Ndikumana


Lucy Avunja Ukimya Kuhusu NdikumanaStaa wa Bongo Movie ambaye kwa sasa anaishi ughaibuni, Lucy komba ameamua kuelezea tuhuma zinazomkabili za kua na uhusiano wa kimapenzi na Hamad Ndikumana, aliekua mme wa msanii mwenzake Irene Uwoya.Akizungumza na gazeti la sani Lucy ameelezea kwamba hakuna jambo lolote linalowakutanisha na Hamad zaidi ya filamu iitwayo "Kwanini nisimuoe" inayohusisha watu wawili tu.
Lucy alisema walipokua wanarekodi filamu hiyo ndio uvumi mwingi ulianzishwa. Ingawa mashabiki wengi walipinga kuwa haiwezekani filamu nzima ikahusisha watu wawili tu na kwamba hao wawili wanauhusiano lakini Lucy amesema kwamba filamu hiyo ikitoka itatoa majibu yote na amewasisitiza mashabiki wainunue filamu hiyo ya "kwanini nisimuowe".

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname