MICHUANO ya COSAFA inatarajiwa
kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 mwaka huu katika viwanja
vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini Afrika
Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana
zikiwa ni nchi waalikwa.
Kuelekea katika michuano hiyo,
kiungo mshambuliaji wa Simba na Taifa Stars, Ibrahim Ajib ‘Mido’
amemshukuru kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic kwa kumuamini na kumpa
nafasi iliyosababisha kocha wa Taifa Stars, Mholanzi, Mart Nooij
amjumuishe kwenye kikosi kilichopo Afrika kusini.
‘Kwanza napenda kutanguliza
shukurani kwa mwenyezi Mungu. Pia napenda kutoka shukuruni zangu kwa
kocha Goran (Kopunovic) aliyeniamini na kunipa nafasi mpaka nimefikia
hapa nilipo”. Ajib ameuambia Mtandao huu kutokea nchini Afrika kusini.
Pia nyota huyo kinda amesema
anajipanga kutumia vyema nafasi ya COSAFA kufanya maajabu endapo atapata
nafasi katika kikosi cha kwanza cha Stars.
“Hapa nilipofikia sio mwisho,
nikipata nafasi huku nilipo (Afrika kusini) nitafanya maajabu makubwa
kwa uwezo wa Mungu”. Amesisitiza Ajib.
No comments:
Post a Comment