Sasa kama Rais alifikia kukodi ndege toka Afrika Kusini maanake alianza kunusa harufu za uasi toka kwa watu wake,ambao pengine angekuja na ndege ya Serikali kwayo Marubani wake ni Wanajeshi wangeweza kumuhujumu kwa namna yoyote ile.Hii kukodi ndege ya nchi nyingine na kuendeshwa na marubani ambao ni raia wa nchi nyingine ya Afrika kusini ndio imemuokoa jana Rais Pierre Nkurunzinza,laa sivyo kama angekuwa amekuja na ndege ya Serikali ya Burundi basi historia ya mwaka 1994 ingejirudia jana ktk uwanja wa ndege wa Bujumbura kwa Nkurunzinza kuripuliwa na ndio ingekuwa mwanzo wa machafuko kati ya wale wanaomuungu Nkurunzinza na wale wasio watiifu kwake
Kwenye usafiri wa anga kuna kitu wanaita "Call Sign",huu huwa ni muito wa ndege au utambulisho wake inapokuwa ktk safari zake,utambulisho huu unaweza kuwa ni namba ya usajili ya ndege,au jina la kampuni ya ndege au jina "mahalia" linaloambatana na "flight number"...kwa mfano wa jina "mahalia" kwa ndege za shirika la umma la Afrika Kusini ni "springbok",huyu ni mnyama mwenye sifa na heshima kwa S.Africa,British Airway wao ni "Speedbird",wakati mashirika kama Fly 540 hujiita kama "swift Tango" n.k
Kwa mfano Tanzania shirika la ndege la fast jet "call sign" yake hujiita kama "Greybird" kutokana na picha ya ndege wa kijivu kama alama ya ndege pale mkiani mwa ndege zao.Kwa hiyo hata watu mashuhuri duniani huwa na "call sign" zao wawapo angani au ardhini iwe tu ni ndani ya ndege,mfano Rais wa Marekani akiwa ndani ya ndege ya Rais "call sign" yake huwa ni "Air Force One", akiwa ndani ya meli ataitwa kama "Marine One";kwetu hapa Tanzania ndege ikiwa imebeba rais hujitambulisha kama "Tanzania One",akiwa makamu wa Rais "Tanzania Two" na akiwa Waziri mkuu rubani huita "Tanzania Three".
Tukirudi kwenye mada ya Nkurunzinza Pierre,jana wakati akiondoka Bujumbura kuja Tanzania hakujitambulisha kama "Burundi One" bali marubani wa kukodiwa toka Afrika Kusini waliita kwa "Call sign" ya "ZS-OPR",kitu ambacho kilifanywa kuwa siri ya nani alikuwa ndani ya ndege hiyo,kwa aina ya usajili wa ndege maadui wa Nkurunzinza iliwawia vigumu kujua hasa ni nani yupo ndani ya ndege hiyo na wasingefanya lolote sababu usajili wa ndege ilikuwa ni Afrika Kusini
Mara baada ya mkutano hapa DSM,Nkurunzinza alitaka kurudi kwa lazima Bujumbura ili akahutubie Taifa kupitia Radio na Tv za Serikali,kujiamini kwako kulikuwa na sababu ya aina ya ndege aliyotumia ili kutua ktk uwanja wa Bujumbura,kitu ambacho aliamini maadui zake hawawezi "kuitungua" kwa sababu zifuatazo:
(1)Ilikuwa ni ndege ya kiraia toka Afrika Kusini
(2)Ilikuwa ndege inayoongozwa na marubani raia wa S.Afrika.
Kuitungua ndege hii yenye marubani wa Afrika Kusini tena "raia" waliombeba "mteja" aliyeikodi,ingeamsha mgogoro mpya wa kidiplomasia ambao "maadui" zake wasingeweza kukubali mtego huo
Nkurunzinza aliondoka Dar es Salaam milango ya saa 1815hrs,lakini baada ya kama saa moja na nusu alirudi tena kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dsm,hii ni baada ya kujaribu kutua mara mbili katika uwanja wa Bujumbura kwa "Call sign" ya " ZS-OPR" badala ya "Burundi One".Hata baada ya rubani kuulizwa mara kadhaa "status of souls on board" alisisitiza kuwa ni "customers" waliomkodi toka Bujumbura-Dsm-Bujumbura.
Baadae Rubani wa ndege akaambiwa "Clear to land at your own risk"...hii ni baada ya chumba cha waongoza ndege kuwa tayari mikononi mwa wanajeshi wasio watiifu kwa Nkurunzinza,hali hii ilimfanya Rubani kugeuza na ku-opt Entebbe International Airport,ambapo Mseven hakuwa tayari,ndipo Pierre akaamua kurudi kwa "Baba" zake Tanzania,mpaka sasa hajulikani amefikia sehemu gani ktk jiji la Dsm,hata Waziri Membe alipooulizwa leo kuwa Nkurunzinza yupo Tz sehemu gani,hakutaka kusema mahali alipo
Hiki ndio kitu pekee kilichomuokoa Brother Nkurunzinza,vinginevyo maadau zake waliokuwa wamefunga mipaka na kutawala viwanja vya ndege wangefanya lolote endapo tu ndege aliyokuwa anatumia ingekuwa ni ile ya Rais ambayo huitumia mara kwa mara,maana kwa maadaui zake kurudi kwa Nkurunzinza toka Dsm na kuhutubia Taifa ingekuwa ni pigo kwani ingezuia vuguvugu na harakati za kumuondoa madarakani zilizokwisha anza.
Lakini mbadala mwingine kama Nkurunzinza angekuwa ametumia ndege ya Rais kurudi Bujumbura kwa kulazimisha ni ima maadui zake wangeitungua ndege yake au wangeruhusu itue na kumshikiria Pierre kwa nguvu,lakini kwa sababu ya "mbeleko" ya ndege ya "kiraia" yenye marubani " raia" toka nchi ya Afrika Kusini,Maadui zake walizingatia diplomasia ya kimataifa na kumsihi rubani asitue Bujumbura "if and only among the souls on board,the soul of Nkurunzinza was boarded"...hii ndio ilikuwa nafuu ya Bro Nkurunzinza na "ujanja" wa team yake ya kijasusi,vinginevyo leo tungekuwa tunaongea mengine na pengine kama yale ya mwaka 1994 ambapo baada ya mkutano wa Dsm,watu walipokuwa wanarudi Makwao wakatunguliw
No comments:
Post a Comment