Mwigizaji wa Origino
Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),akipewa maelekezo ya kuendesha
Trekta mara Baada kukabidhiwa ufunguo wake na Fundi Mkuu wa Kampuni ya
Farm Equip Tanzania , Yunusu Nsekela wakati wa kukabidhiwa Matrekta
kwaajili ya kilimo jijini Dar es Salaam leo
Mwakilishi wa muigizaji
Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa
sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar
es Salaam leo.
Mwakilishi wa muigizaji
Josef Shamba(Vengu),ambaye hakuweza kufika kupokea Trekta lake kwa
sababu ya Maradhi yanayomsumbua akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink jijini Dar
es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji
wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akisalimiana mara baada
ya akimkabidhi ufungua wa Trekta lake Mwigizaji wa Origino Komed, Isaya
Mwakilasa(Wakuvanga) jijini Dar es Salaam leo.
Mwigizaji wa Origino
Komedi ,Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee) akishukuru kwa niaba ya
waigizaji wa kundi la Origino Komedi mara baada ya kukabidhiwa Funguo
za Matrekta ya Kilimo jijini Dar es Salaam leo, kutoka kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif
Sheink,Isaya Mwakilasa(Wakuvanga ),Lucacy Mhavile(Joti) na kulia ni Alex
Chalamila(Mackregani).
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji
wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink akizungumza na Vijana wa
Kundi la Origino Komedi mara baada ya kuwakabidhi funguo za Matrekta
ya kilimo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji
wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink , katika picha ya pamoja
waigizaji wa kundi la Origino Komedi na nyuma yao ni Matrekta ambayo
wamekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda akizungumza katika makabidhiano ya Matrekta ya
Kilimo kati ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Farm Equip
Tanzania,Arif Sheink na Waigizaji wa kundi la Origino Komedi, leo jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya Matrekta ya
Kilimo ambayo waigizaji wa Kundi la Original Comedi wamekabidhiwa leo
jijini Dar es Salaam. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Na Avila kakingo,Globu ya Jamii.
WAIGIZAJI wa kindi cha
Origino Komedi wamewaasa vijana kutumia vipaji vyao ili kutengeneza
maisha yao kuwa mazuri na sio kufikiri kuwa vijana wengi hushikwa mkono
na mtu ili kufanikiwa.
Hayo yamesemwa na kundi
la waigizaji wa Origino Komedi wakati wa kukabidhiwa Matrekta ya Kilimo
aina ya Sonalika kutoka kampuni ya Farm Equip Tanzania jijini Dar es
Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji
wa kampuni ya Farm Equip Tanzania,Arif Sheink amesema kuwa vijana
wameamua kufanya jambo la maana kwa jamii ,"kwani wamenunua matrekta kwa
ajili ya kilimo,vijana wengi wamekuwa wakinunua magari ya kifahari
bila kujua kunakesho na keshokutwa kwa maendeleo yao",alisema Bwa Arif.
Nae Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda amewapongeza vijana wa kundi hilo kuwa kufanya
maamuzi sahihi na ya maendeleo kwa kununua Matrekta hayo kwaajili ya
kilimo,amesema kuwa uamuzi wao ni mzuri hata kwa jamii kwani pia kwa
namna moja ama nyingine itasaidia kuongeza ajira kwa vijana,kwakuwa
kilimo kinahitaji watu wengine na sio wao wenyewe watakao weza kuendesha
Matrekta hayo mashambani.
Kundi hilo la Origino
Komedi linaundwa na vijana 7 ambao ni Alex Chalamila(Mackregani),Josef
Shamba(Vengu),Mjuni Sylivery(Mpoki,nyani Mzee),Lucacy Mhavile(Joti),
Isaya Mwakilasa(Wakuvanga),Emmanuel Mgaya(Masanja mkandamizaji) na
Davidi Seki.
Waigizaji hao wameahidi
kupoleka Matrekta yao kwenda kubeba takataka katika Wilaya ya Kinondoni
ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atazindua kampeni ya
Ona aibu, ambayo itahamasisha usafi katika Wilaya ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment