Mwanzoni mwa mwaka huu (2015) mrembo na muigizaji wa filamu,
Elizabeth “Lulu” Michael aliwa-surprise watu wengi pale alipomzawadia
mama yake nyumba aliyojenga Kimara, jijini Dar es- Salaam.
Lulu alimpa zawadi hiyo mama yake kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa January, 2015.
Je Lulu aliwezaje kufanya mambo makubwa kama hayo katika umri mdogo
na kwa kipato cha kuigiza peke yake? Hayo ni maswali ambayo wengi
walijiuliza, kiasi cha kuwafanya wengine waamini kuwa labda amehongwa.
Lulu amesema kuwa nyumba hiyo alianza kuijenga kidogo kidogo miaka
minne iliyopita kwa kile alichokuwa anakipata kupitia kazi yake ya
uigizaji, lakini watu wengi hawakufahamu mpaka siku alipoitoa kama
zawadi kwa mama yake.
“Kiukweli ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni
nyumba ya chini ya kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba
leo nikipata laki nampa mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu
mtu hajui atashangaa Lulu kapata wapi hela za vuuup, lakini ni kitu
ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata miaka minne..kwahiyo mtu
atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu ataanza kusema
kahongwa hajui background.” alisema Lulu kupitia The Sporah Show
No comments:
Post a Comment