15 May 2015

HIVI NDIVYO RAIS WA BURUNDI ALIVYO POKELEWA KWA SHANGWE KUBWA NCHINI BURUNDI

Mnamo 13 mwezi May jenerali mmoja wa jeshi alitangaza katika redio ya taifa kwamba rais wa Burundi amepinduliwa na kwamba serikali ya mpito itabuniwa.
Lakini msemaji wa rais alikana habari hizo akidai kuwa kulikuwa na usaidizi mdogo katika jeshi kwa mapinduzi kutendeka.


16.20pm-Nurunziza awasili Bujumbura

Rais Pierre Nkurunziza amewasili katika makao ya rais mjini Bujumbura kupitia msafara mkubwa wa magari .Alikaribishwa na umati mkubwa wa wanachama wa chama chake ambao walikuwa wamevaa mavazi ya bendera za chama hicho huku wakicheza densi.

Mwandishi wa BBC Ruth Nesoba ametuma picha za wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza kufuatia kuwasili kwa rais huyo katika ,mji mkuu wa Bujumbura











Mashahidi wameiambia BBC kwamba rais Pierre Nkurunziza amerudi kwao huko Ngozi nchini Burundi na amekuwa akiendeshwa katika gari lilo wazi upande wa juu na kwamba raia wamemlaki kwa shangwe na vigelegele



Shirika la habari la AFP limeripoti kwamba rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerudi nyumbano kwao huko Ngozi yapata kilomita 140 kazkazini mwa mji mkuu wa Bujumbura kulingana na duru ambazo hazikutaka kujulikana zilizo karibu na kiongozi huyo.''Aliwasili katika eneo la Ngozi siku ya Alhamisi.Ni hapa ambapo anatarajiwa kulihutubia taifa kuhusu jaribio la mapinduzi lililofeli'',.AFP lilimnukuu aliyetoa habari hizo.



Kiongozi wa kundi la kiraia linalopinga hatua ya rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu amewataka raia nchini humo kuendelea na maandamano kulingana na shirika la habari la AFP.
Vital Nshimiriman amesema kuwa licha ya kundi hilo kupinga jaribio hilo la mapinduzi,vile raia walivyowashangilia wanajeshi wa jaribio hilo kulionyesha kwamba kuna hamu kubwa ya mabadiliko.



Burundi
Nukuu muhimu kutoka kwa Gervais Abayeho,msemaji wa rais Pierre Nkurunziza akizungumza na kipindi cha BBC cha Newsday.''Mapinduzi hushirikisha watu wengi Kuna wanajeshi wa nyadhfa za chini ambao wamesalimu amri na ambao wanawasaidia maafisa wa poisi na uchunguzi wao,lakini ninaamini watu waliopanga mapinduzi hayo ,wale viongozi hilo ni swala jingine ni lazima washtakiwe.hakuna mgawanyiko katika jeshi.Iwapo unaweza kuwaangalia wale waliokuwa wakipanga kutekeleza mapinduzi ni wachache ...kundi dogo la jeshi'',alisema..


Maandamano yaliokuwa yakiendelea nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza
Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wamekamatwa.
Hatahivyo kiongozi wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare ametoroka na anasakwa kulingana na msemaji wa rais.
Awali Jenerali Niyombare alikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa amerudi nchini Burund na kwamba anatarajiwa kulihutubia taifa.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname