14 May 2015

BASATA WALAANI KITENDO CHA SHILOLE KWA PICHA ZA AIBU ULAYA




Tarehe: 14/05/2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiimba kwa hisia nchini Ubelgiji.Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini limeona picha chafu na zisizo na maadili za Msanii Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole alipokuwa akifanya onesho lake nchini Ubeligiji hivi karibuni.


Katika picha hizo ambazo zimelaaniwa na watanzania wengi nchini kupitia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii, Shilole anaonekana akiwa Jukwaani huku viungo vyake vya sehemu za siri vikiwa hadharani na zaidi akionesha tabia ambazo kwa kiasi kikubwa zimefedhehesha na kuidhalilisha sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla.


BONYEZA HAPA KUONA VIDEO NA PICHA SHILOLE ALIVYOMWAGA RADHI>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname