KIMENUKA! Siku chache baada ya habari ya staa wa Bongo Fleva
anayesumbua na wimbo wa Shikorobo, Nurdin Bilal ‘Shetta’ kudaiwa kulala chumba
kimoja na mwigizaji Rose Ndauka kuandikwa gazetini, mkewe Neila Yusuf
ameshindwa kuvumilia na kudai talaka yake, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Alhamisi iliyopita, Shetta na Rose waliripotiwa na gazeti
‘dugu’ na hili la Amani kuwa walilala katika chumba kimoja katika Hoteli ya
Kingway iliyopo mkoani Morogoro walipokuwa wamekwenda kwenye mazishi ya muasisi
wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya gazeti hilo
kusambaa mtaani na mke wa Shetta kufikishiwa nakala yake na wapenda ‘ubuyu’, kilinuka
ile mbaya nyumbani kwa Mbongo Fleva huyo, Kijitonyama jijini Dar ambapo
mwanamke aliamua kudai talaka yake.
Mke huyo wa Shetta ambaye wamebahatika kupata mtoto mmoja na
msanii huyo (Kayla) alimjia juu mumewe na kutaka amwambie ukweli wa habari hiyo
jambo lililoleta tafrani hadi kufikia hatua ya kutimka nyumbani hadi wazazi wa
pande zote mbili wakalazimika kuweka vikao vya usuluhishi.
Licha ya jitihada hizo kutoka kwa wazazi, bado mama Kayla
alikataa kusuluhishwa na kudai hasira zake zitashuka mara atakapokutana na Rose
uso kwa uso.“Kilinuka kiasi cha mke wa Shetta kufungasha virago huku
akisisitiza kwamba kabla ya kuondoka mazima atahakikisha anamfungia kazi Rose
ili aweze kumweleza kinaga ubaga juu ya ilikuwaje akapindua na mumewe chumba
kimoja,” kilisema chanzo.
Wanahabari wetu walimtafuta Rose na kumuuliza kama amepata
taarifa za kutafutwa na mke wa Shetta na kuhusu kuhusishwa na tukio hilo ambapo alijibu kuwa
hajapata taarifa.“Mimi sijapata hizo taarifa, kama
ananitafuta mimi nipo tu maana sijafanya kosa lolote. Kama nilivyosema awali,
kweli nilisafiri na Shetta kwenda Morogoro na tulilala hoteli moja lakini
vyumba tofauti, Shetta namheshimu siwezi kufanya naye jambo kama hilo,” alisema Rose.
Mapaparazi wetu baada ya kumalizana na Rose, walimvutia waya
Shetta ili kujua ukweli wa tukio hilo
ambapo alikiri kumtokea na kuwashushia lawama wambeya.“Ni kweli mke wangu
amekerwa sana
na habari zile, kuna wambeya ndiyo wamemjaza maneno kiasi cha kuleta tafrani
hadi wazazi kuingilia kati ingawa mimi naamini haya ni mambo ya kifamilia tu
ambayo mke wangu atayaelewa na yataisha tu.
“Mke wangu ni muelewa sana, nampenda na ananipenda, hii hali
ni ya kawaida kwa wanandoa ila kwa kuwa mimi ni msanii mke wangu atajua tu kuwa
watu wanaongea sana juu yetu,” alisema Shetta.
No comments:
Post a Comment