14 April 2015

HII HAPA ORODHA YA MARAIS WAREFU ZAIDI DUNIANI, YANI HUWEZI AMINI.

presKila siku watafiti wana habari mpya kuhusinana na maisha, tumeona tafiti nyingi zikifanywa zikiwemo za magari, majumba watu maarufu, zote zikiwa ni sehemu ya maisha yanayotuzunguka kila siku
Lakini sikuwahi kufikiri kwamba kuna siku nitakutana na utafiti unaozunngumzia urefu wa maraisi duniani.

Leo nakusogezea utafiti uliofanywa January 4, 2015 ambao unazungumzia  marais 10 ambao ni warefu zaidi duniani:-
1. Filip Vujanovic
filip
Papa Benedict xvi akiwa na Rais wa Montenegro ambaye ndiye rais mrefu kuliko wote duniani, ana urefu wa futi 6.5
2. Nicolas Maduro
nico
Huyu ni Rais wa Venezuela, anashika nafasi ya pili kwa kuwa rais mrefu, ana urefu wa futi 6.3
3. Bashar Al- Assad
sha
Huyu ndiye Rais wa nne kwa urefu duniani kutoka Syria, ana urefu wa futi 6.2
4. Stephen Harper
stev
Huyu ni Waziri mkuu wa Canada, ana urefu wa futi 6.2
5. Toomas Hendrik Ilves
ilve
Huyu ni rais wa Estonia ambaye pia aliwahi kuwa mwandishi wa habari, ana urefu wa futi 6.2
6. Paul Kagame
kaa
Kwa Afrika huyu ndiye rais anayeongoza kwa urefu, lakini duniani anakamata nafasi ya sita kwa futi 6.2 huku binti yake akimzidi kwa kuwa na futi 6.6
7. Barack Obama
obb
Barack Obama ni Rais wa Marekani, ana urefu wa futi 6.1 huku mke wake Michelle Obama akiwa na futi 5.11
8. David Cameroon
two
Huyu ni Waziri mkuu wa Uingereza, urefu wake haujatofautiana na wa Rais Obama wa Marekani, wote wana futi 6.1
9. Blaise Compaore
U.S. President Barack Obama and First Lady Michelle Obama With W
Huyu ni Rais wa Burkina Faso ambaye Oktoba mwaka jana aliamua kujiuzulu kutokana na machafuko nchini kwake, ana urefu wa futi 6
10. Recep Tayyip Erdogan
TURK
Huyu ni rais wa Uturuki aliyekabidhiwa madaraka mwaka jana, ana urefu wa futi 6

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname