14 April 2015

ZITTO ASHIRIKI MAZISHI YA WALIOFARIKI KWA KUUNGUA MOTO AJALI YA BASI NA LORI


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe aliyeshika tama wa tatu kutoka kulia akiwa pamoja na wananchi wa kijiji cha Ruaha wilayani Kilosa wakati wa mazishi ya miili watu 15 walioteketea kwa moto baada ya kutokea ajali ya basi la Kampuni ya Nganga kugongana na lori katika kijiji cha Masimba tarafa ya Mikumi mkoani Morogoro juzi. Watu 19 walikufa katika ajali hiyo. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Ngwira
MWENYEKII wa Chama cha  ACT-Wazalendo, Anna Mghwira,amesema ubinafsi
unaofanywa na viongozi wa serikali ndiyo chanzo kikuu cha migogoro
katika maeneo mbali mbali ya nchi
Mghwira alitoa kauli hiyo jan mjini Morogoro wakati akihutubia mkutano
wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa ndege mjini hapa na kueleza
kuwa ni wakati wa viongozi kusimamia maslahi ya wananchi badala ya
kufikiria familia zao
Alisema viongoi wengi wamejilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi  na
kukodisha kwa wawekezaji huku wakiwaacha wananchi wakigombea maeneo
machache yaliyosalia hali inaowafanya wakulima na wafugaji kila moja
kumuona mwenzie ni adui
“Hawa wanajificha katika mgongo wa uwekezaji kwa kuchukua maeneo
makubwa kishakuwakodisha wananchi ACT wazalendo tutapiga  marufuku
wawekezaji kuwakodishia ardhi wakulima ili kummilikisha mkulima ardhi
yake"alisema Mghwira
kwa Upande wake kiongoziwa Chama hicho Zitto Kabwe alisemakupuuzwa kwa
misingi iliyoachwa na muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius
Nyerere ndiyo chanzo cha kufa kwa viwanda vingi nchini
Alisema njia nzuri ya Kumuenzi Mwalimu Nyetrere  ni kukataa
ubinafsishaji holela, kwa kuwa ujamaa  na ulijenga viwanda. Mfumo wa
sasa umeuza viwanda na watu hawana ajira
Aliongeza kuwa  Ujamaa ulikuwa na faida zaidi kuliko hali ya sasa.
“ACT Wazalendo itamuenzi Mwalimu kwa kupinga sera za ubinafsishaji sio
kama chama chetu kitataifisha mali za watu hilo hapana ila
itarekebisha makosa anunuzi hawajatekeleza mikataba yao,”
Zitto alisema sababu ya kuachwa kwa misingi hiyo ndiyo iliyoisukuma
chama cha  ACT- Wazalendo kuamini  katika misingi ya Nyerere inayoleta
usawa wa kidemokrasia na kuimarisha uchumi wa kila Mtanzania.
“Mwalimu Nyerere aliipenda Morogoro kwa kuigeuza kuwa mkoa wa viwanda,
lakini leo hii viwanda vya Sukari asilimia  50 hapa na hakuna kiwanda
kipya cha Sukari tofauti na vilivyojenga na Mwalimu.
“Mtibwa, Kilombero, Kagera na TPC Moshi vyote vilijengwa enzi za
mwalimu, lakini leo hii viwanda vinapata ushindani mkubwa kutokana na
uagizaji wa Sukari kutoka nje ya nchi na hata kuzuiwa viwanda vipya
kujengwa,”alisema.
Kiongozi huyo alisema pamoja na kujengwa viwanda hivyo kujengwa bado
vimekuwa vikiwanyonya wakulima wa miwa na hivyo kupelekea kilimo chao
kutowafaidisha. Wakulima wa miwa kwa mfano wananyonywa kwenye bei na
hawana haki ya kujua thamani ya muwa wao.
Alisema chama cha  ACT-Wazalendo inataka kupiga marufuku uagizaji wa
Sukari bila kodi, huku akishauri kuanzishwa kwa viwanda vidogo vya
miwa na wananchi wanaolima miwa wote kuwa na hifadhi ya jamii ili
kuweza kuboresha maisha yao ya sasa na baadae.
“Hata hivyo Sukari nchini haitoshi kwani uwezo wetu ni kuzalisha tani
300,000 wakati mahitaji ni tani 500,000. Ili kuhakikisha bei ya Sukari
inakuwa himilivu ACT inapendekeza viwanda vya Sukari kupewa bei nafuu
ya umeme kama ruzuku,” alisema
Akizungumzia namna Mkoa wa Morogoro unavyochangia katika pato la Taifa
(GDP), Zitto, alisema unashika nafasi ya sita kati ya mikoa 21ya
Tanzania Bara lakini bado upo chini kwa maendeleo.
Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kaskazini, alisema kwa mujibu wa
takwimu  za taarifa ya Maendeleo ya watu Tanzania (THDR) ya mwaka
2014, ambao walitumia hesabu za uchumi za 2012.
“…lakini Mkoa wa Morogoro upo chini kwenye maendeleo ya watu wake
ambapo unashika nafasi ya 11. Elimu ni changamoto kubwa ambapo katika
kila watu 100 wa wa mkoa huu ni watu wanane  tu ndio wana elimu ya
Sekondari,” alisema

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname