05 March 2015

AENDA JELA KWA KUWAHI KUFIKA KAZINI MAPEMA

Kevin McGill anatarajiwa kwende jela wiki 14.
Mwendesha lori la kuzoa taka kwenye majumba ya watu mji wa Sandy Spring jimbo la Georgia nchini Marekani anatakiwa kwenda jela wikiendi 14 kwa kisa ni kuwahi kuchukua taka mida ya saa 11 asubuhi badala ya saa 1 asubuhi.na kuwapigia watu kelele wakiwa wamelala.
Kervin McGill yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi baada ya kusomewa mashitaka kwamba anapochukua taka saa 11 asubuhi anawapigia kelele waliolala na inakua usumbufu kwa wengine na majirani hao walijaribu kuifungulia kampuni yake Kervin McGill lakini wao walisema sisi hatuondeshi hilo lori, na ikabidi kibao kimgeukie yeye na kuhukumiwa kwenda jela wikiendi 14.

Kesi hiyo imewasitua watu wengi na kuchukua headline kwenye vyombo vya habari huku wengi wao wakiwa wameshikwa na mshangao wa mtu kwenda jela kwa sababu ya kuwahi kufanya kazi yake. Mtu kama huyu alistahili kupata onyo sio kwenda jela. Hakimu alimwambia Kervin McGrill kuanzia sasa anatakiwa achukue taka saa 1 asaubuhi na saa 1 usiku tu na si vinginevyo.

1 comment:

  1. Pata bongo flava mbali mbali - http://rubega.com//index.php?a=explore

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname