25 March 2015

Vita ya Ray C na Zamaradi Yapamba Moto



Wale Mastaa waliodaiwa kuingia kwenye bifu zito, Zamaradi pamoja na Ray C, na baadae kupatana, huku chanzo cha bifu kikidaiwa kuwa ni mwanaume, bifu hilo limeibuka tena, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni maneno ya kejeli ya mtangazaji zamaradi mketema kwa mwanamuziki Ray C.

Hivi karibuni Zamaradi aliposti picha ya mwanae kwenye mtandao wa Instagram akim wish Happy birthday, uku aki repost baadhi ya pongezi kutoka kwa baadhi ya mastaa na mashabiki mbali mbali wa mtangazaji huyo, kitendo ambacho kilitafsiriwa kuwa mwiba kwa mwanamuziki Ray C ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto.

Mtangazaji huyo ambaye baadae tena aliandika comment kwenye page yake, akiwauliza mashabiki wake ni kitu gani ambacho wanatamani kuwa nacho katika maisha lakini hawana? Au wengine wanavyo na vinawafanya wawe na furaha?

Comment hiyo ilizua utata uku baadhi ya wadau wakidai lile lilikuwa dongo kwa hasimu wake wa mda mrefu ray c ambaye mpaka sasa hajabahatika kupata mtoto wala kuolewa, ndipo team Ray C ilipoamua kumtag boss wao huyo ambapo Ray C hakutaka kulaza damu na kuamua kujibu mapigo kwa mtindo ule ule wa vijembe, hali iliyozua balaa uko Instagram na kuziacha team hizo mbili zikishambuliana kwa matusi ya nguoni.
“Bitchez be like (Marry Me can't u see am pregnant again)????????(Players be like(In your Dreams keep popping dem kids!!!!)lol!”-Ray C aliandika

Ray C baada ya kuona hali inakuwa mbaya, alihoji kama Zamaradi ndiye mwanamke pekee aliyezalishwa bila kuolewa apa duniani? Aliwataka watu waache kuhisi vitu ambavyo hawana uhakika navyo.
Mpaka sasa bado Zamaradi ambae siku ya jana amejifungua motto wa pili hajazungumza chochote kuhusu varangati hilo.
By Warumi-on JF

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname