Tabia
ya baadhi ya wanafunzi kupenda kuigilizia majibu wakati wa mitihani si
jambo la ajabu lakini kwa kilichotokea nchini India kimeweza kuchukua
headlines kwa kiasi kikubwa.
Udanganyifu wa mtihani umekuwa jambo la kawaida katika Jimbo la Bihar na kuna picha mpya zimetolewa zikionyesha tukio hilo likifanywa kwa kiwango kikubwa.
Wazazi na marafiki wa wanafunzi hao
walipigwa picha wakipanda ukuta wa vyumba vya kufanyia mitihani ili
wawape majibu wanafunzi katika mitihani kwenye moja ya shule za upili
nchini humo.
Mpiga picha Dipankar ambaye alipiga picha hizo katika wilaya ya Saharsa
amesema alipoingia katika chumba cha mtihani na kuchukuwa picha hizo
wanafunzi hawakujali nakuendelea na kuigilizia majibu waliyopewa na
ndugu zao.
Tayari baadhi ya wanafunzi waliohusika
na udanganyifu huo wamefukuzwa shule huku wazazi wao wakifunguliwa
mashtaka na bado uchunguzi unaendelea.
Mtihani huo ulioandaliwa na bodi ya shule ya Bihar (BSEB) ulianza Jumanne na unatarajiwa kuendelea hadi tarehe March 28.
No comments:
Post a Comment