ISHU ya uchawi kwa wanawake wajawazito ndilo suala kubwa linaloingia
kwenye hisia za baadhi ya watu hasa mimba inapokuwa changa, hofu hiyo
sasa imemwingia mwandani wa Mbongo-Fleva anayeuza zaidi kwa sasa, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’
ambaye anadaiwa kuikimbia Bongo kwa muda ili mimba yake isije
kuchoropoka kama ilivyokuwa kwa akina Wema Sepetu na Penniel Mungilwa
‘Penny’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa familia ya
Diamond, hivi karibuni Zari aliondoka Bongo mara tu baada ya kurejea
kutoka Zanzibar walikokuwa wameenda kula bata katika Msimu wa Valentine.
Chanzo hicho kilidai kwamba, wakati staa huyo mwenye maskani yake Afrika
Kusini na Uganda akiwa Bongo maneno mengi yalisemwa na wengine kudiriki
kuwapigia simu watu wa familia hiyo wakimtaka Zari aache tabia ya
kujionesha na ujauzito wake kwani hawajui Wabongo vizuri.
NYUMBANI KWA MAMA D
Ilidaiwa kwamba mmoja wa watu waliokuwa wakiambiwa ishu hiyo
alimfikishia moja kwa moja Zari aliyekuwa akipika na kupakua nyumbani
kwa mama Diamond ‘D’, Sanura Kassim ‘Sandra’ maeneo ya Sinza-Mori, Dar.
Habari zilidai kwamba, Zari aliposikia maneno hayo aliamua kuondoka huku
Diamond akisapoti uamuzi wa mpenzi wake kwa asilimia mia.
HOFU YATANDA
“Alipomwambia Diamond kwamba anaondoka kwa hofu ya mambo ya ushirikina,
jamaa alimuunga mkono na kumsisitiza kutulia kabisa maana majanga kama
hayo Bongo huwa ni ya kawaida na yalishawahi kumtokea kwa Wema na Penny
ambao walishika ujauzito na ulitoka bila kujua sababu za msingi.
“Kweli Zari amekimbia Bongo, baada ya kuona watu wanamfuatafuata kila
kukicha, si unajua Wabongo huwa hawaishiwi maneno? Zari amemtaka Diamond
wakaishi Sauz.
“Watu wamekuwa wakisema vibaya juu ya uhusiano wake na Diamond, hasa
kipindi alipokuwa Zanzibar, hivyo baada ya kurudi tu aliamua kwenda zake
South (Afrika Kusini) ili akajipumzikie wasije wakampagawisha mimba
yake ikatoka bure.
“Nafikiri mwenyewe unajua namna Zari alivyokuwa maarufu Bongo tangu awe
na Diamond hivyo siku hizi kila anachokifanya utaona wanavyomtolea macho
na wengi wao hawaishi kuudisi ujauzito wake.
YASIJE YAKAWA YA WEMA NA PENNY
“Maana wanasema eti hawezi kuzaa na Diamond, kuepuka maneno kaamua
kujiondokea zake wasije wakamloga bure akashindwa kweli kuzaa na ndugu
yetu kama ilivyoshindikanika kwa Wema na Penny,” kilisema chanzo chetu.
TUJIUNGE NA DIAMOND
Baada ya kujazwa ‘ubuyu’ huo, mwanahabari wetu alimsaka Diamond ili
athibitishe kama kweli kilichochangia Zari kuondoka harakaharaka Bongo
ni kwa sababu ya kuogopa ushirikina ili mimba yake isichoropoke kama
inavyosemwa, jambo ambalo Diamond aliishia kuguna huku mdogomdogo
akifafanua.
“Ujue Wabongo wana maneno sana na mara nyingine huwa wanalazimisha uongee hata vitu ambavyo havipo.
“Mimi sina mtoto na natamani sana siku moja niwe naye hivyo ninapokuwa
na mtu naye anaonesha hali ya kunisapoti na nia moja ya kunipa mtoto,
sina budi pia kumheshimu kwa uamuzi wake.
“Kweli Zari aliondoka siku chache tu baada ya kurudi kutoka Zanzibar,
hayupo Bongo, si unajua Bongo mambo mengi inafikia hatua hata kumkatalia
anapotaka kuondoka inakuwa ngumu maana Wabongo wanaongea sana na mara
nyingine wanamfanya mtu kukosa imani na ndiyo maana inafikia wakati
nashindwa kujibizana nao.
“Ninachoamini mimi ni katika Mungu tu, yote wanayosema ipo siku yatapata
majibu maana Zari Kiswahili hajui vizuri hivyo tunaepuka sana watu
kumtumia umbeya na kumtafsiria vitu vingi ambavyo si sahihi,” alisema
Diamond.
No comments:
Post a Comment