MAMA mzazi wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amefunguaka baada kuongea na
FC kuwa moja ya sababu iliyofanya ofisi yake kuhama kutoka maeneo ya
Sinza Meeda ilipokuwa wakati wa uhai wa mwanaye ni gharama za pango hilo
kupanda kila mwaka.
“Kuna watu ambao wanadai na kuandika hata katika mitandao ya kijamii
kuwa eti ofisi za Kanumba The Great Films zimefungwa na hazipo tena, si
kweli kodi ni kubwa sana hivyo tumehamishia Kimara Temboni,”anasema Mama
Kanumba.
Mama Kanumba amesema kuwa ofisi hiyo inafanya kazi wala haijafungwa na
kwa uhakika ni kwamba kuna filamu ambayo imekamilika na itatoka hivi
karibuni chini ya kampuni, filamu hiyo imewashirikisha wasanii Flora
Mtegoa, Mohamed Mwikongi ‘Frank’, Rose Ndauka na wasanii wengine.
No comments:
Post a Comment