Mpenzi msomaji wangu nataka kuzungumzia namna ambavyo usipoangalia unaweza ukamshawishi mpenzi wako akusaliti bila wewe kujua. Nataka kuligusia hili kwasababu, nimegundua kuna watu wanaowapenda sana wapenzi wao lakini bila kujijua wanajisahau na kuwafanya wapenzi wao kukinai penzi lao na kuanza kutafuta mtu mwingine wa kumpatia kila anachokitamani.
Sote tunajua kwamba mapenzi ni kuridhishana, kupeana kile ambacho kila
mmoja alikitarajia kutoka kwa mwenzake. Hata hivyo, sidhani kama yupo
mtu aliye tayari kuwa na uhusiano na mtu ambaye hajui mapenzi zaidi ya
yale ya faragha tu.
Ninachomaanisha hapa ni kwamba, wapo wanawake huko mtaani ambao
wanajisifu kuwa wao ni watundu sana kwenye ‘mambo flani’ lakini
wanashangaa kuona bado wanasalitiwa na waume zao.
Wanawake wa sampuli hii wanaamini kwamba, ukishakuwa mtaalam katika
mambo ya kwenye sita kwa sita tayari ushamshika mumeo na kamwe hawezi
kukusaliti. Jamani huko ni kujidanganya!
Tunapoyazungumzia mapenzi, tunajumuisha mambo mengi.
Kama mwanaume anachokitaka kutoka kwa mwanamke ni mapenzi tu, si angekwenda kuchukua changudoa tu akapewa kila anachokitaka?
Lakini kwakuwa mwanaume anahitaji zaidi ya mapenzi ya kwenye sita kwa
sita kutoka kwa mke, ndiyo maana wanawake wanatakiwa kuwatimizia mambo
mengine ya msingi yanayoweza kuwafanya wakiri kwa kusema ‘Yes! mwanamke
niliyenaye ananitosha kila idara, sihitaji mwingine katika maisha
yangu’.
Ila sasa, mwanaume hawezi kusema hivyo endapo atampata mwanamke anayejua
mapenzi sana lakini, hajui kupika, ni mchafu, hana ukarimu kwa ndugu
jamaa na marafiki, haheshimu ndugu wa mume wala mume wenyewe! Huyu
atakuwa hana sababu ya kumshawishi mwanaume kudumu naye.
Atashangaa licha ya ‘kumtumbuiza’ ipasavyo mumewe bado anasalitiwa au
kutoswa kabisa, kwanini? Kwasababu mwanaume anakosa vitu kadhaa ambavyo
angevipata asingekuwa na tamaa za kijinga.
Nini ninachotaka ujifunze kupitia somo hili la leo? Ishu ya msingi hapa
ni kwamba, mapenzi ya kitandani tu hayawezi kukufanya ukamshika vilivyo
mpenzi wako. Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia.
Unamkuta mwanaume ni mtaalamu wa kupachika magoli wavuni lakini hamjali
mpenzi wake, hamheshimu na wala hampatilizi katika shida nyingine za
msingi isipokuwa penzi tu. Jamani maisha katika uhusiano hayajengwi kwa
tufali moja la mapenzi tu, wanaoamini hivyo ni malimbukeni hivyo kuna
kila sababu ya kubadilika.
No comments:
Post a Comment