05 March 2015

Picha: Wema Sepetu Atoa Baraka kwa tumbo la Aunty!



Mrembo na mwigizaji wa filamu mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii hapa Bongo, Wema Sepetu  ame-share nasi picha kadhaa akiwa na rafiki yake kipenzi, mwigizaji  Aunty  Ezekiel ambae kwa sasa ni mjamzito na karibu kujifungua.
Kwenye picha hizi Wema anaonekana akiwa amelishuka tumbo la Aunty kitendo ambacho kinaashilia kuwa mwanadada huyo alikuwa akitoa baraka zake kwa kiumbe kilichomo ndani mbali na ujumba ambao Wema aliutupia kuonyesha kuwa yeye na aunty ni marafiki  wa kweli na wanafurahia pamoja.
Kitendo hiki cha wema kiliwafurahisha wengi na kumsifu Wema kuwa na moyo wa upendo kwa jamaa zake.
Nami naungana nao kumsifu Wema kwa moyo huu aliouonesha, kwani rafiki wa kweli ni yule ambae mnakuwanae wakati wote…
Mzee wa Ubuyu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname