SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) umemfungia mechi tatu mchezaji wa Mbao FC ya Mwanza, Emmanuel Mseja kutokana na kitendo cha kujisaidia haja ndogo uwanjani huku mpira ukiwa unaendelea.
Mseja alifanya tukio hilo hivi karibuni wakati timu yake ikicheza na AFC ya Arusha katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.Uamuzi huo wa kumfungia nyota huyo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya TFF, pia pamoja na adhabu hiyo amepigwa faini ya shilingi laki moja (100,000).
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema Mseja amepigwa faini hiyo kutokana na kufanya kitendo hicho ambacho kimetafsiriwa siyo cha kiungwana katika michezo.
Wakati huohuo Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo umetangazwa jana (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.Nkamia alisema, TFF pamoja na CRDB kwanza warekebishe kasoro zilizopo katika tiketi hizo za elektroniki.
No comments:
Post a Comment