04 March 2015

Picha: Jinsi mvua ilivyoleta maafa huko Kahama, 50 wasadikiwa kupoteza maisha na 80 kujeruhiwa

Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo imeuwa watu zaidi ya 50 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kahama  Bw Benson Mpesy

Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa 4 za usiku ilidumu kwa muda wa masaa mawili ikiambatana na upepo mkali na mawe yaliyopelekea watu hao kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa na kuharibu mazao  pamoja na miti .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alifika eneo la tukio akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambao wametoa pole kwa wafiwa pamoja na mikakati ya serikali kuangalia utaratibu wa kusaidia kaya zilizobakia.
Hata hivyo bado idadi kamili ya athari kwa ujumla ukiacha vifo vya watu haijatolewa.

Mi naungana na waombolezaji kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki walioondokewa  na ndugu zao katika janga hili.
Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu ...amina.























Na Emmanuel Mlelekwa Kahama

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname