SERENGETI BREWERIES LTD
TAARIFA KWA UMMA
MKAZI WA KOROGWE, TANGA AIBUKA MSHINDI WA
MTOKO WA MBUGANI KWENYE FAINALI YA KAMPENI “TUTOKE NA SERENGETI”
12/03/2015, Dar es Salaam, Droo ya mwisho ya kampeni ya Tutoke na
Serengeti imemshuhudia mkazi wa Korogwe Tanga Bw. Robert Gabriel Moriale akitangazwa
mshindi katika fainali ya kampeni “Tutoke na Serengeti”. Fainali hiyo
imefanyika katika ukumbi wa Baa ya Hongera iliyopo maeneo ya Kijitonyama-Dar es
salaam karibu na chuo cha Ustawi wa jamii.
Mshindi huyo alijipatia
fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambapo ataongozana na mtu
wake yeyote wa karibu kwa muda wa siku tatu huku SBL kupitia bia yake ya
Serengeti Premium ndio itahusika kugharamia usafiri, chakula, malazi sambamba
na fedha taslim za mshindi kujikimu pindi atakapokua safarini.
Akiongea kupitia njia ya simu mara baada ya kutangazwa mshindi wa
mtoko wa mbugani, Bw.Robert (49)alipokea
taarifa hizo kwa furaha na alisikika akishangilia kwa kelele baada ya kuambiwa
kwamba amejishindia “Mtoko wa Mbugani”.
Alipoulizwa kama alishawahi kushinda chochote kabla ya zawadi
hiyo, Robert alijibu “Nimekuwa nikishiriki tangu mwanzo na nimepata bia za bure
nyingi tu pamoja na pungozo la Tsh 300. Lakini hii ya leo kwa kweli
sikuitarajia kabisa”
Akiongea wakati wa kufunga kampeni hiyo, Meneja chapa wa bia ya Serengeti
Premium Lager , Bwana Rugambo Rodney alisema, “Tumefurahishwa sana na ushindi
wa bwana Robert na tunapenda kumshukuru kwa kushiriki na tunaamini aliifurahia
bia ya Serengeti Premium ambayo imemletea furaha ya kipekee siku ya leo.
Rodney pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru washiriki wote kwa
kutumia muda wao wa thamani katika promosheni hii na kuwapa moyo wale ambao hawakubahatika
kushinda mtoko wa mbugani, Bajaj au bia za bure kutokata tamaa na kushiriki
tena nyakati zijazo kwani SBL imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kiasi
cha faida waliyopata kwa wateja wake. Aliongeza kuwa wateja wakae mkao wa kula
kwani kuna kitu kikubwa kinaandaliwa kwa ajili yao.
Wakati kampeni hii iliyodumu takribani miezi minne inafikia
tamati, SBL imetoa shukrani za pekee kwa wateja wake wa Serengeti Premium Lager
baada ya kushuhudia washiriki zaidi ya
milioni moja wakijaribu bahati zao na kuifanya promosheni ya “Tutoke na
Serengeti” kuwa yenye mafanikio kutokana
na muitikio mkubwa na uelewa kutoka kwa wananchi.
Kampeni imewazawadia wateja mbalimbali fursa ya kutembelea mbuga
ya wanyama ya Serengeti wakati wengine wakiondoka na zawadi murua kama vile Limo
Bajaj ambazo kwa kiasi kikubwa zitabadilisha maisha yao. Kulikuwa pia na fedha
taslim za kila wiki, bia za bure, na punguzo la Tshs300 katika kila bia ya
Serengeti Premium.
Promosheni hii ya nchi nzima pia ilipata ushirikiano wa hali ya
juu kutoka kwa B-Pesa, wataalamu wa teknolojia mpya ya usambazaji fedha waliochangia
Limo Bajaj sita kwa washindi mbalimbali. Pia walihusika na usambazaji wa fedha
kwa washindi nchi nzima katika kipindi chote cha miezi mine ya kampeni.
No comments:
Post a Comment