28 March 2015

MCHUNGAJI GWAJIMA AZIMIA WAKATI AKIHOJIWA POLISI

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.Gwajima ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Waandishi wa Mtanzania Jumamosi waliokuwa kituoni hapo wanaeleza kuwa walimuona Gwajima akitolewa kutoka katika chumba cha mahojiano akiwa amebebwa.Kwa mujibu wa waandishi hao Gwajima ambaye alikuwa amebebwa na maofisa wa polisi alipelekwa moja kwa moja kwenye gari aina ya Noah kwa ajili ya kumpeleka hospitali.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa 3:16 usiku lilikuja katika kipindi kisichozidi dakika saba tangu askofu huyo alipoonekana akiwa ameshikiliwa na wasaidizi wake kuelekea msalani huku yeye mwenyewe akiwa amejishika kichwa.SOMA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname