MAAJABU!
Ama kweli dunia ina mambo na ya Mungu mengi! Mwanamke mmoja, mkazi wa
Mbezi- Maua jijini Dar aliyefahamika kwa jina moja la Neema, amelea
ujauzito wake kwa miezi tisa yenye matumaini lakini siku ya kujifungua
akaambulia kiumbe cha ajabu kilichofanana na nyoka aina ya chatu..
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, awali Neema alikuwa akisumbuliwa na pepo
wachafu hali iliyomfanya akatishe masomo ya sekondari na kuanza kwenda
kanisani kila wakati kwa ajili ya maombi.
MAUZAUZA KILA MARA
Chanzo
kilisema kuwa, kipindi chote hicho, Neema alikuwa akianguka na kutaja
majina ya watu wa mtaani anapoishi kwamba ni wachawi, wengine
wanahusika kumchukua yeye usiku na kwenda naye makaburini ambako
humlisha nyama na kumnywesha damu za watu.
“Neema
alikuwa akisumbuliwa na mapepo tangu akiwa mdogo na alikuwa anasumbua
kweli kweli. Alipokuwa akipandisha ‘madudu’ yake hayo hakuna aliyeweza
kumshika labda wanaume kama watano. Pia kuna wakati alikuwa akitaka
kujiua kwa kujichoma kisu,” kilisema chanzo hicho.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Naye
mama mzazi wa Neema ambaye hakupenda kujitambulisha kwa jina,
alipozungumza na mwandishi wa habari huku majirani wakifurika nyumbani
kwake, alisimulia jinsi mwanaye huyo alivyokuwa akiteseka kipindi chote
tangu alipokuwa mdogo mpaka ikafika hatua amepata ujauzito huo na
hatimaye kujifungua kiumbe kinachofanana na chatu.
“Ni
mambo mengi ambayo tumeyapitia lakini siwezi kumkufuru Mwenyezi Mungu
kwa sababu mpaka leo hii tuko wazima japo mitihani ni kipimo cha maisha
na hata hili lililotokea karibuni ni mtihani pia, ila kikubwa ni kuomba
sana.
“Baada
ya kupata huu ujauzito kuna wakati tulikuwa hatulali, akianza kulia ni
usiku kucha, anasema kuna kitu kinambana kifuani. Tulipokuwa tukienda
hospitali kwa ajili ya uchunguzi, vipimo vilionesha mtoto tumboni
hachezi.
“Mimi
kama mzazi, hayo mambo yaliyokuwa yanamtokea mwanangu nilikuwa nayaona
kama maajabu f’lani hivi japokuwa kipindi hicho alikuwa mzima na mimi
mwenyewe nilikuwa nikimsubiri mjukuu wangu kwa hamu, kumbe tunakuja
kupokea kitu cha ajabu namna ile,” alisema mama huyo.
SIKU YA KUUMWA UCHUNGU
Iliendelea
kudaiwa kuwa, kipindi chote cha ujauzito, Neema alikuwa mtu wa maombi,
lakini siku ya kuumwa uchungu alikimbizwa hospitali (haikutajwa jina) na
kujifungua kiumbe cha ajabu. Ndipo familia ikaamua kukaa kikao na
kuamua kukizika kiumbe hicho kama chatu.
Mama
Neema anasema: “Mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu, kilikuwa kama
chatu halafu kina magamba na meno mawili marefu lakini hakikuwa hai.
Tulishtuka sana, tukaona ni mkosi katika familia lakini tuliamua
kukizika kile kiumbe.“Sikuona sababu ya kuwaonesha majirani zangu kwa
kuwa kilikuwa kinatisha. Ila naona ni bora niwape taarifa kuwa, mwanangu
alijifungua kiumbe cha ajabu.”
ALICHOSEMA ALIYEJIFUNGUA
Naye Neema mwenyewe alipozungumza kuhusu tukio hilo la ajabu, alikuwa na haya ya kusema:
“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.
“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.
“Labda
niwaulize mama zangu ambao tayari walishazaa kama tumbo huwa linapanda
juu mpaka kifuani badala ya kushuka? Na nilikuwa nakabwa sana kuanzia
kifuani mpaka kwenye koo, usiku sikuwa nalala kutokana na maumivu
niliyokuwa nikiyapata mpaka nilipojifungua hicho kiumbe.
“Usione
watu tunatembea, hatujijui tuna nini kwenye miili yetu. Leo hii
yamenikuta mimi, kesho mtu mwingine. (huku akiwaangalia majirani) mi
nawaomba ndugu zangu tukazane kumwomba Mungu kwani mimi maombi
yamenisaidia sana.”
Chanzo ni gazeti la Amani via Gpl
No comments:
Post a Comment